Sunday, September 5, 2010

Dk. Slaa aiteka ManyaraDk. Slaa ameiteka Manyara. Na wananchi wa Manyara wamemteka pia. Ilikuwaje? Kwanza, walijaa katika mikutano yake katika majimbo ya Hanang na Mbulu. Pili, walizuia misafara yake kokote alikopita wakitaka awahutubie, walau kwa dakika moja tu! Tatu, walimwahidi kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu kwa kuchagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani. Kipya ni kwamba alitumia usafiri wa Kipanya(Hiace) badala ya helikopta kutoka Babati hadi Mbulu, kwa sababu helikopta ilipata hitilafu kidogo jana Jumatano mara baada ya kutua mjini Babati ikitokea eneo la Bashnet. Katika picha ya kwanza, ni umati ulijitokeza kumlaki Dk. Slaa katika eneo la Haydom, jimboni Mbulu; na katika picha ya pili Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

0 comments:

Post a Comment