Sunday, September 5, 2010

Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod Peter Slaa

Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod Peter Slaa

Dk Willibrod Peter SLAA

1. Anachokisimamia

• Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, uamakini na uwajibikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.

• Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya Dk Slaa Kielimu na Kitaaluma

Dk Slaa ana shahada na stashahada zifuatazo

• Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome

• Stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari

• Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari

• Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho

4. Mafanikio ya Dk Slaa Kikazi na Kitaalamu

Dk Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:

• Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wasioona Tanzania, 1992-1998

• Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991

• Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 1977-1979 na 1982-1985.

• Padri wa Kanisa ikatoliki kuanzia 1977 hadi 1991.

5. Vitabu alivyoandika

• Utimilifu wa Msichana (1977)

• Utimilifu wa Mvulana (1977)

• Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981)


6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo: Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk Slaa Kisiasa

Dk Slaa ana uzoefu wa muda mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo:

• Mbunge wa Karatu kwa miaka 15, kutoka 1995 hadi 2010

• Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa

• Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998-2002

• Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk Slaa Kitaifa na Kimataifa

Dk Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo

• Mjumbe wa kuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika, Carribean na Pacific-EU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996-2000

• Mjumbe Kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

• Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010

• Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la SADC (Inter Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010

• Naibu Kiongozi wa Kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

• Mwenyekiti, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania, 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

• Dk Slaa amekuwa mbunge wa Karatu kwa miaka 15 mfululizo. Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye mafanikio makubwa ikiwemo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii. Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka

15 ya ubunge wa Karatu kwa ajili ya taifa zima.

• Ndiye Katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA. Kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

• Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kashfa za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki Kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.


10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa

• Kuanzisha mchakato wa kuandika upya Katiba ndani ya siku 100 baada ya kuunda serikali

• Kupambana na kuwashughulia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

• Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bora na cha kisasa, chenye faida na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha na kuuza mazao mbalimbali.

• Kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika ngazi zote.

• Kuanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya pensheni kwa wastaafu

• Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa mishahara inapanda kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda.

Chagua Mabadiliko,

Mchague Dk Slaa ili arudishe tunu za taifa letu: Uzalendo, Maadili, Uadilifu na Umakini.

0 comments:

Post a Comment