Saturday, September 18, 2010

Dk. Slaa Katika Kampeni

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea wa ubunge katika jimbo la Karatu kupitia chama hicho, ambaye ni mridhi wake, Mchungaji Israel Natse, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu janaMgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu leo. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni zake kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Bariadi juzi. Picha na mdau Joseph Senga wa Tanzania Daima.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kumi katika vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Kagunga na Zashe kata ya Kagunga,Mjini Kigoma hivi karibuni.kina Mama wa kata ya Kagunga mkoani Kigoma wakiimba nyimbo za kumsifu mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni.
mmoja wa wazee wa kata ya Kagunga akiongea katika mkutano huo wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazi,Zitto Kabwe.
wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Kagunga wakiwa wamefurika kwa wingi kumsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazi,Zitto Kabwe alipokua akihutubia katika mkutano wa kampeni.

0 comments:

Post a Comment