Thursday, November 11, 2010

BLOGU YA MARAFIKIWACHADEMA

Karibuni kwenye blogu ya marafiki wa chadema Gonga www.marafikiwachadema.blogspot.com wale wote wenye mapenzi na chama hichi wanaopenda kuchangia maendeleo yake , kutupa habari picha na vitu vingine vingi karibuni sana

GONGA KWENYE FOLLOW UTAWEZA KUTOKEA HABARI NA MAMBO MBALIMBALI YA CHADEMA KWENYE BARUA PEPE YAKO

Wednesday, November 10, 2010

DR SLAA ALIPOTINA BUNGENI

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Chadema Dr,Wilbroad Slaa akisalimiana na baadhi ya wabunge katika jengo la bunge leo jijini Dodoma

Friday, November 5, 2010

Maandamano- uchaguzi tanzania jumamosi nov 6washington dc 2010

Ndugu Watanzania ambao tunaoshi maeneo ya Washington DC, tunawatangazia wote kwamba tutafanya mandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, 2010 na namna shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi zilivyofanywa na Tume ya Uchaguzi wa Tanzania ambao uligubikwa na wizi na udanganyifu wa hali ya juu katika sehemu na maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Kwa kuwa State Department imetoa ridhaa ya maandamano haya ya amani, tunawaomba Watanzania, wanayoipenda Tanzania, sehemu yoyote walipo hapa Washington DC, Maryland, Virginia na Pennsylvania wajitokeze kwa wingi, wake kwa waume, watoto na kumbuka kuja na bendera, mabango, ngoma, zeze na vinubi, Tshirts ili message ifike kwa Presedent Obama.

Tunawaomba watanzania wote waishio Marekani mujitokeze kwa wingi katika kupinga matendo hayo ya ubadhilifu nchini kwetu. Kwa wale ambao wanataka kujitokeza wasiliana nasi kwa: #202 367 2761 begin_of_the_skype_highlighting 202 367 2761 end_of_the_skype_highlighting # 301 655 6577 begin_of_the_skype_highlighting 301 655 6577 end_of_the_skype_highlighting # 224 628 8279 begin_of_the_skype_highlighting 224 628 8279

Wednesday, November 3, 2010

Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

http://mwananchi.co.tz/

Tuesday, November 2, 2010

TAMKO LA DR SLAA

Nawashukuru wote mliojitokeza kupiga kura na kukipa chama chetu ushindi wa kukumbukwa, ushindi wa kihistoria mkikaribisha mapambazuko mapya ya uongozi katika taifa letu. Kama ilivyokuwa kwenye matokeo ya Ubunge matatizo yamehamia kwenye matokeo ya Urais na kutokana na unyeti wa nafasi hii tunahitaji uangalifu katika kushughulikia. Msife moyo kwani tukiwa tayari muda si mrefu ujao tutazungumza nanyi kwa taarifa zaidi.

Dr. Wilbrod Slaa | Facebook

WASHINDI WA UBUNGE CHADEMA 2010 - 2015

 1. Halima James Mdee -Kawe/Chadema
 2. Tundu Lissu - Singida Mashariki/Chadema
 3. Mustapha Quorro Akonaay- Mbulu/Chadema
 4. Israel Yohana -Karatu/Chadema
 5. John Mnyika -Ubungo/Chadema
 6. Silinde David -Mbozi Magharibi/Chadema
 7. Salvatory Naluyaga Machemuli-Ukerewe/Chadema
 8. Ole Sambu -Arumeru Magharibi/Chadema
 9. Joseph Mbilinyi -Mbeya Mjini/Chadema
 10. Philemon Ndesamburo Kiwelu-Moshi Mjini/Chadema
 11. Dk Antony Mbasa -Biharamulo Magharibi/Chadema
 12. Joseph Selasini -Rombo/Chadema
 13. Hezekiah Wenje -Nyamagana/Chadema
 14. Peter Msigwa -Iringa Mjini/Chadema
 15. Freeman Mbowe -Hai/Chadema
 16. Vincent Nyerere -Musoma Mjini/Chadema
 17. Godbless Lema -Arusha Mjini/Chadema
 18. Zitto Kabwe/C -Kigoma Kaskazini/Chadema
 19. Hayness Samson -Ilemela/Chadema
 20. John Shibuda -Maswa Magharibi/Chadema
 21. Meshack Opulukwa -Meatu/Chadema
 22. Sylvester Kasulimbayi Mhoja-Maswa Mashariki/Chadema
 23. Regia Mtema / Chadema
 24. Prof Mlambiti /Chadema

JOHN SHIBUDA - MASWA MAGHARIBI

Mh. John Magale Shibuda (pichani) na Silvester Kasulumbayi wametangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi kuwa wabunge wa maswa magharibi na mashariki kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu.

PETER MSIGWA - IRINGA MJINI


MGOMBEA wa chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amevunja ngome ya CCM mkoa wa Iringa baada ya kuwabwaga vibaya wapinzani wake katika matokeo ya ubunge baada ya kujizolea kura 17742 dhidi ya kura 16916 alizopata mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Monica Mbega ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

GODBLESS LEMA - ARUSHA MJINI

Pichani ni Mbunge mteule wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Godbless Lema akiwa anaondoka katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge akiwa anasindikizwa na wanachi pamoja na wapambe wake. Mh. Lema amepata kura 56, 569 dhidi ya Dk. Batilda Burian wa CCM aliepata kura 37,460. Picha na Woinde Shizza

ZITTO KABWE - KIGOMA KASKAZINI

Zitto Kabwe kwa tiketi ya CHADEMA amelitetea jimbo lake la Kigoma Kaskazini

JOHN MNYIKA - UBUNGO

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hivi sasa ni kwamba Mgombea Ubunge kwa jimbo la Ubungo na Naibu katibu mkuu kupitia chama cha CHADEMA,Bwa.John Mnyika ametangazwa rasmi kuwa ndiye Mbunge mteule wa jimbo hilo.

FREEMAN MBOWE - CHADEMA HAI

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ameshinda uchaguzi Jimbo la Hai na kurejea bungeni tena kama mbunge baada ya kuwa nje kwa miaka mitano.