Thursday, September 16, 2010

Kampeni za John Mnyika Mgombea Ubunge - Ubungo

Mkutano wa Mburahati

Baada ya kupita vichochoro na mitaa toka Magomeni Kagera hadi Mburahati, nilifanya mkutano wangu katika uwanja wa Mburahati pembeni kidogo mwa kituo cha Polisi.

Nashukuru wanahabari ambao mara kwa mara wamekuwa wakijitokeza katika mikutano yangu

Mgombea Udiwani Kata ya Manzese, Alhaji Kabunda akifanya mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Channel 5 "EATV"

Baada tu ya kumaliza mkutano wangu wa hadhara Mburahati niliweza kufanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha Channel 5 "EATV"

Mkutano wa Magomeni Kagera

Nikihutubia Mkutano wa Magomeni Kagera


Alhaji Kabunda akihutubia na kusisitiza jambo, pembeni yangu ni mgombea udiwani mwanamke pekee katika jimbo la Ubungo-Farida Momba.

Wakati mwingine tunahakiki nyaraka vizuri na kujadiliana. Ni kashfa za uuzaji wa viwanja vya wazi katika jimbo la Ubungo. Kashfa ambayo niliianika hadharani kupitia mkutano wa Magomeni Kagera

Kamanda Kotide akifanya vitu vyake kabla ya hotuba kuanza. Ni miongoni mwa hazina ya makamanda wenye karama ya uimbaji ndani ya CHADEMA.

Alhaji Kabunda, Mgombea Udiwani Kata ya Manzese

Umati wa Wananchi wa eneo la Magomeni-Kagera wakifatilia mkutano wangu.

Mtaa kwa Mtaa, Kichochoro kwa kichochoro

Kuna wakati mwingine napenda sana kuwafata wananchi wangu katika maeneo yao haswa. Hapa natembea katika mazingira yao ya kila siku, yaani mitaani na vichochoroni kabisa. Nakatiza toka Magomeni Kagera ambako nilimaliza mkutano wangu wa hadhara kuelekea Mburahati.

Nashukuru sana wananchi ambao walikuwa wanajitokeza toka majumbani na kuja kunilaki!pia nawashukuru sana wale wote ambao waliungana nasi mpaka Mburahati ambako nilihutubia.
"Mheshimiwa kichochoro hiki kitatufikisha mapema na kwa urahisi zaidi"

Nilishuhudia wakina mama wakijitokeza na watoto wakiwa wamewabeba wakija kuniangalia na kunisabahi.Nawaomba kama mlivyojitokeza, tafadhali mjitokeze kwa wingi sana ninyi na marafiki zenu(shosti) wote katika kunipigia kura Oktoba 31, 2010.


Hawa walinipa hamasa na faraja sana pale walipoona msafara wangu unakuja kwa miguu waliponyoosha alama ya "V" alama ya CHADEMA!

0 comments:

Post a Comment