Thursday, September 30, 2010

Dk Slaa azungumzia mambo makuu matatu

Viti Maalumu

Kwanza amezungumzia suala la Viti Maalumu kupitia CHADEMA, akaweka wazi kilichoazimiwa na Kamati Kuu ya chama. Majina 105 kati ya 147 ya walioomba kuteuliwa viti maalumu, yamepitishwa; na sasa yatapelekwa Tume ya Uchaguzi kama sheria inavyodai. Walioteuliwa hawakutajwa majina kwa waandishi. Mfumo wa uteuzi ulizingatia vigezo sita (6) vilivyoainishwa na mtaalamu aliyeteuliwa na chama hicho ili kuifanya kazi hiyo, Dk. Kitila Mkumbo. Vigezo hivyo ni 1. Kiwango cha Elimu. 2. Uzoefu wa kazi ya kisiasa. 3. Uzoefu wa uongozi nje ya siasa. 4. Kugombea Jimbo. 5. Mchango wa mgombea katika chama na kampeni zinazoendelea. 6. Umri wa mtu katika chama. Kila kipengele kilikuwa na vigezo vidogo vidogo kama vinne, vyenye alama tofauti. Na kwa mujibu wa Dk Slaa na Kitila, viti hivyo vimetawanywa nchi nzima, kwa kuzingatia vigezo hivyo hivyo. Akahitimisha kwa kusema: "Ingawa kuna usemi kwamba siasa ni mchezo mbayan, kwa Chadema, siasa ni sayansi na unachezwa kisayansi." Alitumia pia fursa hiyo kusisitiza kuwa Chadema kimeweka wagombea 185 ambao ni ziaidi ya asilimia 75 ya wagombea ubunge nchi nzima; na kwamba idadi hiyo kinatarajia kuvuna wabunge wa kutosha, na kiko tayari kuunda serikali.

Usalama wa Taifa

Dk. Slaa alitumia fursa hiyo kutamka kwamba ana taarifa za kikachero kuwa Rais Kikwete ameagiza wana usalama wa taifa wasambae nchi nzima kuhujumu uchaguzi. Akasisitiza kwamba, "kwa sura ya sasa, Kikwete ameshashindwa...na amani ya nchi ikivurugika, Kikwete ndiye atabeba lawama na laana.." Alisisitiza pia kuhusu waraka uliosambazwa nchi nzima ukiwataka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchi nzima kufanya kila wawezalo kulazimisha ushindi wa CCM. Akasema hujuma hii inaweza kusababisha umwagaji damu, na kwamba asingependa itokee.

Utafiti na vitisho vya Synovate

"Tunasubiri kusikia Synovate wamefungua kesi. Kama hawajaenda, waende sasa. Wasipofanya hivyo tutawaharibia credibility yao hapa nchini na kimataifa. Chadema tunapofanya kitu chetu huwa haturudi nyuma. Hatuna woga. Gazeti lililoshitakiwa nalo lisiwe na woga." Baada ya hapo alionyesha vielelezo vya utafiti uliofanywa na Synovate, ambao katika kipengele GPO 6 liliulizwa swali: "Kama ucahguzi ungefanyika leo, nani ungempigia kura ya urais?" ambalo Synovate walikanusha kwamba halikuwamo katika utafiti wao, wakidai wanataka kuufanya baadaye kabla ya uchaguzi mkuu. Ukweli ni kuwa walifanya utafiti lakini CCM iliingiza 'mkono' wake baada ya kubaini kuwa matokeo hayo yalikuwa yanaonyesha Kikwete yuko nyuma ya Dk Slaa.

Tahadhari ya Mbowe

Freeman Mbowe alitoa tahadhari kwa Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, na Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema wamepewa mamlaka ya umma, ambayo wakiyatumia vizuri wanaweza kulipeleka taifa kwenye amani, na wakifanya makosa wanalitumbukiza kwenye ghasia. Akasema kinatokea sasa, CCM wameshindwa siasa za majukwaani, na watatu hawa wako katika mikakati michafu ya kuvuruga uchaguzi. Akasema kama wanatakua kuugeuza uchaguzi wa uchakachuaji, hapatatosha! Aliwaomba Watanzania kuwa tayari kulinda maamuzi yao, kura zao. Akasisitiza: "Tunaomba Watanzania na jumuiya ya kimataifa mtuelewe..."

2 comments:

Unknown said...

CCM wanatapatapa na hakika hawana pa kushika ndio maana wamehamishia majeshi kwenye vyombo vya usalama na hiyo yote ni kuonyesha kutoungwa mkono na wananchi wengi walio amka maana CCM mtaji wao mkubwa uko wa wananchi wengi wenye uelewa mdogo na hatamu za nchi hii. Kwa kifupi umbumbumbu wa wananchi ndio mtaji mkuu wa CCM

Wamekuwa mstari wa mbele kutumia siasa chafu kwa kuvituhumu vyama vya upinzani kuwa vikishika dola vita poteza amani ya nchi iliyokuwepo au itagawa wananchi ba hivyo kujenga matabaka katika jamii, wanajua fika kuwa hiyo ni ghiriba maana hakuna chama kinachogombea ili kivunje amani, kama vyama vingine viko kimya na kuendeleza kampeni makini kuwatumia au kutumia vyombo vya usalama maana yake nini? Nani kati ya CCM na wapinzani anayetaka kuharibu amani ya nchi?

Mimi naona pia kuna haja waraka huo wa kikachero usambazwe kwenye vyombo vya habari ili wananchi wapenda amani wajue uovu unaofanywa na CCM kupitia taasisi zetu ambazo zinamhusu kila raia wa Tanzania bila kujalisha itikadi za kichama.


Mtoi

Anonymous said...

KWA NINI CCM INAKWEPA MDAHALO?
Kunaweza kutafsiriwa ifuatavyo.
1. Kulwepa mdahalo ni kutokujali hoja za watu na kung'ang'ania zako tu.
2. Ni kuonyesha kuwa hauko tayari kusikia maoni wala maswali ya wengine.

3. Ili kuweza kujua mgombea atakayetimiza matakwa ya wapiga kura wake ni kwa njia ya kuulizwa maswali na kujibu hoja anazopewa.
4. Mgombea anaponadi tu ilani ya Chama chake bila ya kuweza kueleza uwezo wa binafsi hawezi kuaminiwa na wananchi kwani hatujui kama ni kweli anaamini ilani ambayo pengine hakushiriki kuitunga.
5. Uwezo wa mtu na yaliyomo akilini na moyoni mwake hujulikana kwa namna anavyoweza kueleza msimamo wake wa binafsi juu ya hoja.
6. Kushindwa kuhudhuria midahalo ni kutaka kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
7. Hata kama mbuzi aliyeko kwenye gunia anafaa lakini kwa kuwa huna uhakika naye ni afadhali umchukie unayemuona na uliye na hakika ya unachoweza kuvuna toka kwa mbuzi huyo.
NI AFADHALI KUJUA KUWA MBUZI WAKO ATATOA MAZIWA KIDOGO KULIKO ALIYE KWENYE GUNIA AMBAPO UNAWEZA KUKUTA NI BEBERU. WA maziwa Kidogo anaweza kuzaa. WENGI WANAOGOMBEA KWA CHADEMA KAMA SIO WOTE WAMEONEKANA KUWA NI WENYE MAZIWA (TIJA) KWA UWEZO WAO WA KUSIMAMIA HOJA NA UNAONA USONI MWAO KUWA WANA UCHUNGU UTOKAO MOYONI.
MSINUNUE MBUZI KWENYE GUNIA.
KIKWETE NAYE JE ATAWEZA KUWA RAISI WA TANZANIA
1. RAISI Kikwete HAWEZI KUONGEA ZAIDI YA DAKIKA. 10 kwa kipindi hiki. Akichaguliwa ni nani ajuaye kuwa itafikia mahali ziwe dk. 5 tu.
2. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni kupuuza watanzania kwa kutokujali.
3. Kule kuzidishiwa nguvu ya majini bado hajakanusha na tunasikia ameendelea kuanguka ila haitangazwi.
4. Kama kweli tunampenda rais Kikwete tumtakie maisha marefu aounguziwe majukumu mazito kama ya uraisi. Nawaomba wananchi tumpendao rais tujali afya yake.
MATAMSHI YAKE YANAONYESHE KUFICHA JAMBO KWA WANAOJUA SAIKOLOJIA.
5. Wako wanaosema kuwa rais ananyanyapaa watu wa ukimwi kwa kusema ni kiherehere chao.
6. Na hata watoto kupata mimba wakiwa mashuleni ni kiherehere chao.
7. Watu wanaweza kufikiri kwa kuwashambulia wanaoogua ukimwi kwa mtu mwenye heshima ya uraisi ni kujaribu kufikisha ujumbe fulani wa kuficha jambo fulani.
TAFADHALI KUONYESHA UPENDO WETU KWA RAISI WETU TUMPUMZISHE KWANI NI VIGUMU YEYE KUTAKA KUPUMZIKA.
Ni KAMA MTOTO MDOGO KUMPELEKA KWENYE SINDANO HAPENDI. INABIDI UMSHIKE KWA NGUVU.

Post a Comment