Mgombea Ubunge wa jimbo la Hai kupitia chama cha CHADEMA ,Freeman Mbowe akiwasalimia baadhi ya wakazi wa Moshi mjini jioni hii wakati wa maandamano yao kabla ya mkutano wao wa kampeni walioufanya mjini humo jioni ya leo.
Gari ya baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA wakisindikizwa na wakazi mbalimbali wa mjini moshi jioni hii wakati wa mkutano wao wa kampeni walioufanya leo kwenye uwanja wa Mashujaa mjini humo.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha CHADEMA,wakati Dr Slaa alipokuwa kihutubia jioni ya leo kwenye uwanja wa mashujaa mjini humo.
Kaka ,
Hili ni nyomi la DK. Slaa sasa hivi ama kwa hakika watu ni wengi,wengi sana , picha zinajieleza zenyewe, maana hata muda wa kuweka maelezo naona napitwa kaka. Eneo ni uwanja wa mashujaa moshi mahali alipofanyia pia JK. Unazoziona wakiwa juu ya gari ni mwenyekiti Mbowe na muingine ni Dk. Slaa mwenyewe. Hapo walikuwa katika maandamano makubwa hapa mjini na walikuwa wanapita mbele ya ofisi za CCM wilaya ya moshi mjini kwa kishindo na chopa yao ikiwa juu. Leo imesambaza vipeperushi kwa gharama ya sh 500,000/ kwa ushuru wa kuchafua mji
hapa moshi.
Mdau wako Louie

NB: Nakushukuru sana mdau wangu Louie kwa uharaka wa kunitumia picha hizi,pamoja na kwamba ulikuwa ukikosa uhondo wakati mwingine,lakini haukujali sana badala yake ukaona pia ni vema sehemu ya jamii ione mambo yaliyokuwa yakiendelea jioni ya leo mjini humo kwa picha hizi,ama kwa hakika nakushukuru sana.Haya Wadau wengine popote pale mlipo Mlango uko wazi wa kupokea picha zozote zile, ili mradi zisichafue hali ya hewa na pia zizingatie maadili,zitakwenda hewani bila kupendelea kwa namna yoyote ile.
Hii ndiyo nchi yetu basi na tuijenge pamoja-Asanteni kwa ushirikiano wenu,
JIACHIE.!
Hii ndiyo nchi yetu basi na tuijenge pamoja-Asanteni kwa ushirikiano wenu,
JIACHIE.!
0 comments:
Post a Comment