
Pichani ni mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama cha CHADEMA,Bw.Ally Khalfa Mleh

Mgombea  Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh.Zitto Kabwe akisisitiza jambo  wakati alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma  Mjini,Bw.Ally Khalfa Mleh wakati wa  uzinduzi wa kampeni za chama hicho   mjini humo katika uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema   jana.

Wanachi waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho

Mgombea  Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh.Zitto Kabwe akiwahutubia  wananchi wa Kigoma Mjini wakati wa uzinduzi wa kampeni wa chama hicho  mjini humo katika uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema  jana.

Wanachadema  kabla ya uzinduzi rasmi wa kambeni yao ndani ya Kigoma Mjini kwenye  uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema jana.

Wagombea  Udiwani wa chama cha CHADEMA katika picha ya pamoja mjini Kigoma wakati  wa kutambulishwa rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwenye  uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema jana.

Mgombea  Ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia chama cha CHADEMA akiwasili na  mgombea mwingine wa chama chake kupitia jimbo la Kigoma mjini,Bw.Ally  Khalfa Mleh kwenye uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema  jana.

Baadhi ya watu wakiwemo wanachama wa chama CHADEMA waliojitokeza uwanja hapo kusikiliza mchakato mzima wa sera za chama hicho .

Pichani  ni uzinduzi rasmi wa kampeni  ya chama cha CHADEMA ndani ya Kigoma  Mjini kupitia  mgombea wa kiti cha Ubunge,Bw.Ally Khalfa Mleh kwenye  uwanja wa Community Center,Mwanga,Kigoma mjini mapema jana.
 
0 comments:
Post a Comment