Thursday, September 2, 2010

Upinzani haumezi matapishi.. DK.Slaa aitoa shoo serikali ya JK


Mbunge wa Karatu, na Naibu kiongozi wa Upinzani, Dk. Wilbroad Slaa, leo alionekana dhahiri kumpiga kijembe mbunge wa Bariadi mashariki John Cheyo wakati aliposema kazi ya upinzani si kuipigia makofi CCM .
Mbunge huyo machachari wa Chadema alitumia muda wake jana wa mchango kuishambulia ipasavyo CCM na kukosoa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tatu na kusema haijaleta maisha bora kwa kila Mtanzania, kama ilivyodai.
Dk.Slaa Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani alifafanua kwamba badala ya wananchi kupata maisha bora, maisha yamewashinda huku bei ya bidhaa muhimu zikiwa Juu.
Alisema wananchi wengi wameacha kunywa chai kwa vile sukari sasa imekuwa bidhaa ya anasa na bei imepanda kutoka Sh. 1,200 hadi Sh. 1,800 huku mkate nao ukiwa umepanda maradufu. Alisema mwaka 2005, mkate ulikuwa Sh. 500 hadi Sh. 600 na sasa inakimbilia Sh. 1,500 hadi Sh. 2,000.
Alisema hali imekuwa ngumu kwa kuwa bei ya kila kitu imepanda mara dufu wakati kipato cha Mtanzania imebaki palepale huku nguvu ya mwananchi ya kununua bidhaa na huduma ikishuka kutokana nna kuporomoka kwa thamanin ya Shilingi.

0 comments:

Post a Comment