Wednesday, September 8, 2010

Friends of Slaa - MKUTANO MUHIMU

Wana FOS wote,

Napenda kuwataarifu wote kuwa tunapendekeza kufanya kikao cha wana FOS wote siku ya Iddi Pili (Kwa maana hiyo itategema na muandamo wa mwezi, lakini ni Iddi Pili, hivyo Iddi pili yaweza kuwa ni Friday au Saturday kutegemeana na na muandamo wa mwezi) saa kumi kamili bila kuchelewa. Mkutano utafanyika Landmark. Nelson Mandela Road. Kutakuwa na agenda muhimu sana.

Tunaendelea kupokea michango. Napenda kuwashukuru wote mnaochangia. Kwa wale ambao bado kwa heshima na taadhima naomba tukamilishe michango yetu. Ndugu zangu vitu hivi viwili vinahitajika sana; tunahitaji finances ili tuweze ku implement activities tulizokubaliana. Lakini pia tunahitaji manpwer au volunteers kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinahitaji nguvu kazi, moja ya kazi muhimu ni kulinda kura, kuwa mawakala na kuhamasisha vijana, kina mama na wengine wote ili tumpigie kura Dr Slaa aweze kurejesha Tunu za Taifa na hili ni kwa maslahi ya wanyonge wote wakiwamo wana CCM. Hili halina maslahi kwa mafisadi tu.

Hivyo naomba, mnipe mawazo yenu iwapo mnaafiki siku, mahali na saa ya kufanya mkutano huu. Pia iwapo mngependa nifafanue au nieleze agenda ingawa naona ni vizuri tukazijadili katika kikao. Kwani wakati mwingine jukwaa hili linaweza lisiwe zuri sana kueleza hayo. Naomba mawazo yenu.

Naomba pia mjiunge na group email ya frinds of Slaa kama inavyoonekana hapo juu. Muhimu naomba mumtumie Yona friendsofslaa@gmail.com taarifa za wapi mnatoka, na contacts zenu ili tuweze kuratibu masuala mbalimbali. Tunataka kujua eneo unalotoka, email na namba yako ya simu.

Njooni tuje tupange ili tuweze kufanikisha mikakati yetu.

Kwa wanaotaka kuchanga unaweza kuchanga kupitia MPESA, ZAP na account namba ya CRDB. Namba zipo ktk blog ya marafiki wa slaa.

Tembelea Friends of Slaa | FOS | au Gonga Friends of Slaa - Movement 4 Change | Google Groups

0 comments:

Post a Comment