Thursday, September 9, 2010

Dr slaa akiwasili mjini shinyanga na helikopta yake tayari kwa kampeni


e Mgombea Urais Kupitia Chadema Mheshimiwa Dk Willibrod Slaa leo ameingia mkoani Shinyanga kusaka kura za urais kwa kishindo.Na Helikopta yake imeanza kazi upya baada ya kufanyiwa matengenezo madogo kwa siku nne zilizopita.

1 comments:

Ng'wana said...

Kwanza kabisa namwombea Mungu Dr. Slaa, Rais mtarajiwa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu ni mwaminifu!

Wajibu wetu: Wakati tukimtakia heri sana Dr. Slaa, isiwe tu kwa nia, bali kwa kuhakikisha tunampigia kura zetu na kuzilinda, kwani wadanganyifu na mafisadi wanaishi kati yetu. Kulinda si lazima kukesha kwenye eneo la kura siku ya uchaguzi. Mipango michafu huanmza mapema zaidi kabla ya hapo. Hivyo ukisikia, kuona au kugundua mipango yoyote michafu (kama vile hifadhi ya kura batili za ndiyo) arifu umma mapema - hali ilivyo siku hizi ki-mawasiliano ni rahisi kuawaambia watu wenye mapenzi mema).

Haki ya Umma: Wapiga kura wanayo haki ya msingi kuwapima kwa kina na kuwalinganisha wagombea. Ingawa wanapata fursa kwenye mikutano, bado ni muhimu wagombea kufanya mdahalo wa pamoja, jambo ambalo wagombea viti vya ubunge majimboni limekuwa likifanyika. Tunataka wagombea Urais nao wawe kwenye mdahalo wa pamoja na wapiga kura wao, ili wapate nafasi ya kuiwahoji. Tunasikitika kujua kuwa chama-tawala kimekataa midahalo kwa hofu ya kuulizwa maswali (hususan juu ya ufisadi) mbayo hawana majibu yake; lakini waambiwe wazi kuwa mdahalo kama sehemu ya mchakato kuelekea uchaguzi ni lazima na wala si hiari.

Wakizidi kukataa, basi tunaomba Dk. Slaa apewe muda wa kutosha katika vyombo vya habari (TV na Redio) ahutubie taifa, ili watu wapate kumfahamu zaidi ikiwa ni pamoja na waliopewa rushwa na wenginewe wanaoendelea kudanganyika; kwa sababu, kwa mwelekeo wa sasa, yeye ndiye tumaini zaidi na mwenye nafasi kubwa ya kuwa Rais wetu.

2011 HATUDANGANYIKI

Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania

Post a Comment