Thursday, August 19, 2010

WARAKA WA WAZI KWA WATANZANIA

Ndugu Mtanzania,
> >
> > Naomba kuwasilisha kwako waraka huu ukiwa ni mwamsho na na hamasa kwetu kama
> > Wananchi na Taifa ili kulikwamua taifa letu kutoka katika hali mbaya ya
> > kiuchumi tuliyonayo inayoenda sambamba na kuzorota kwa Uongozi na Utawala
> > bora.
> >
> > Matatizo ya Tanzania yamegawanyika katika makundi makubwa mawili ambayo
> > ukiangalia kwa kina, yanaoana na kila moja kinategemea mwenziwe. Matatizo
> > haya ni Uchumi (Umasikini, Ujinga na Maradhi) na Uongozi (Utawala holela,
> > Uzembe, Rushwa, Uvivu, uwajibikaji).
> >
> > Naomba upokee waraka huu kupima nafsi yako na wale watakao kuja kwako kuomba
> > kura yako wakati wa uchaguzi, uwe ni wa Serikali ya Mitaa, Wabunge au Urais.
> > Nakusihi utumie mwamko na hamasisho hili kujihoji nafsi kuwa wewe binafsi
> > una nafasi gani na nguvu zako zina nafasi gani ili kuleta msukumo utakaoleta
> > maendeleo ya kweli na kulikwamua Taifa kutoka kwenye shida zinazotuzingira
> > na kutudumaza. Kutumia waraka huu, jiulize kwa makini ni nini maana ya
> > Maendeleo na ni maendeleo ya namna gani Watanzania wanayataka na
> > yatawasaidia vipi wao na vitukuu vyao.
> >
> >
> > Miaka 10 iliyopita niliandika haya yafuatayo hapa chini kama ningekuwa
> > mgombea Uchaguzi Mkuu 2000. Nayarudia tena kwa kuwa ni katika haya kumi (10)
> > ndivyo Mipango ya Maendeleo kwa mujibu wa mawazo na maoni yanaweza kutumika
> > kama nyenzo na dira kutukwamua kama Wananchi binafsi, jamii na hata Taifa.
> >
> > · Kurudisha na kuimarisha Heshima, Utu na Uadhi ya Mwananchi na
> > Taifa la Tanzania
> >
> > · Kurudisha na kuimarisha Heshima, Wajibu na Hadhi ya kazi na
> > kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini
> >
> > · Kuelimisha Wananchi haki zao kama raia, wajibu wao na sehemu yao
> > katika Taifa na Serikali yao kupitia Katiba, Serikali Kuu, Bunge na Mahakama
> >
> > · Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga,
> > Umasikini, Njaa na Maradhi

TEMBELA WWW.WANABIDII.NET KWA MJADALA ZAIDI

0 comments:

Post a Comment