MGOMBEA Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema dr. Wilbroad Slaa amesema endapo atashinda urais katika uchaguzi mkuu wa oktobar mwaka huu jambo la kwanza atakalolishughulikia litakuwa ni kuboresha mishaharana maslahi ya walimu,askari polisi na wafanyakazi wa kada mbalimbali nchini.
Dr. Slaa amesema hayo mjini Morogoro jana katika mkutano wa hadhara wa kuomba kudhaminiwa kuwania urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Chadema.
Amesema amekuwa akistaajabu kuona wabunge wakilipwa fedha nyingi wakati askari wanaowalinda wananchi na mali zao wakilipwa mishahara na maslahi duni licha ya kufanyakazi katika mazingira magumu
Aidha amesema endapo atafanikiwa kuingia Ikulu suala lingine atakalolipa kipaumbele cha kwanza ni suala la maslahi ya walimu ili waweze kufanyakazi yao vizuri na kuboresha taaluma nchini.
Naye mfuasi wa chama hicho mwanasheria mashughuli nchini bw. Mabere Marando amesema muda wa kampeni utakapofika ataueleza umma wa watanzania namna viongozi wa ccm walivyoshirikiana kwa maslahi yao binafsi kukwapua fedha katika akaunti ya madeni ya nje
Amka Na BBC
44 minutes ago
0 comments:
Post a Comment