Thursday, August 19, 2010

prf.Mwandosya arudisha fomu

Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Rungwe Ndg. Noel Mahyenga akimkaribisha Prof.Mark Mwandosya alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kurudisha Form za kugombea Ubunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki
Prof Mark Mwandosya na waliomsindikiza wakimsikiliza Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Rungwe Ndg. Noel Mahyenga Ofisi kwake mara baada ya kufika hapo kurejesha form za kugombea Ubunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.
Anaewania Ubunge kupitia CCM Jimbo la Rungwe Mashariki Prof. Mark Mwandosya akiangalia mda mara baada ya kutaniwa na mwenzie anaewania jimbo la Rungwe Magaharibi Prof. Mwakyusa kuwa mda wa kurudisha form umekwisha katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Rungwe alipokuwa anakwenda kurudisha form ya kuwania Kugombea Ubunge wa Jimbo hilo
Muwania Ubunge kupitia CCM Jimbo la Rungwe Mashariki Prof. Mark Mwandosya akiwa ameongozana na mke wake na baadhi ya wana CCM kuelekea Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Rungwe kurudisha form ya kuwania Kugombea Ubunge wa Jimbo hilo.

1 comments:

Anonymous said...

Hii blog inasema ni ya marafiki wa Slaa au kuna makosa katika hilo? Ajabu ni kuwa leo ni siku muhimu sana kwa Slaa mwenyewe kwa kuwa amerudisha Fomu za kugombea Urais wa Jamhuri, cha ajabu hakuna habari zinazoelezea hilo, badala yake kuna picha za akina Mwandosya na Kikwete wanarudisha fomu. Sielewi, kama haiwezekani kutoa updates, basi haina haja ya kupiga kampeni ya JK hapa, sisi wengine hata kuona picha yake tunapoteza MOOD! Jaribu kutoa updates kuhusu Slaa sio hao wengine!

Post a Comment