Tuesday, August 10, 2010

Marekebisho ya Katiba Zanzibar

Kinachofanyika Zanzibar ni uhuni, uhuni wa baadhi viongozi ambao kwanza
hawakuwepo wakati swala hili la Muungano likiwakilishwa ktk baraza la
Mapinduzi. Wengi wao hawakushiriki hata kupitisha artical of Union
naifahamike wazi kwamba sii kweli madai ya baadhi viongozi kwamba Muungano
ulipangwa na Nyerere na Karume tu. Haya sii kweli kwani toka mwanzo mbali na
Karume, Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi
walishiriki kikamilifu kama wawakilishi wa Visiwani ktk kuunda Muungano. Na
hata report ya Nyalali commission ilieleza wazi kwamba Artical of Union
ilikupitishwa na Baraza la Mapinduzi.

Kero ya wananchi sio Uhalali wa Muungano hata kidogo hizi ni politics za
kina Seif isipokuwa ni nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano. Wananchi kama
watotowa Muungano huu wanataka kujua urithi wao, haki yao na kwa nini
wanakosa baadhi ya huduma ambazo watoto wengine (bara) wanazipata. Lakini
haya ya kuulizia ndoa yetu hayana faida wala maslahi kwa Wazanzibar kwani
wakisha kuwa NCHI watafaidika kipi zaidi ya leo hii walivyo?

Kwa hiyo, kinachofanyika leo hii ni kuhoji uhalali wa ndoa ambayo wewe na
mimi ni watoto walozaliwa ndani ya ndoa hii. Where and how they hook up
wazazi wetu iwe ni udadisi tu wa kutaka kuijua historia yetu na sio kutafuta
mbinu ya kuvunja ndoa. Hao kina Shariff Hamad ni watu wa Hizbu hawakushiriki
isipokuwa wamepewa undugu kuoa ndani ya familia hii. Seif know nothing about
Union zaidi ya kupinga kwa sababu alikuwa nyuma ya Sultan hali huyo Karume
bado anatumia mbinu za marehemu Baba yake kujilinda yeye na maslahi ya
familia yake.

Na sina maana hawana haki ya kuuliza swali lolote liwe la legitimacy, au
nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano (artical of Union) laa hasha wanayo
haki hiyo na zaidi ya kuuliza ikiwa watafuata sheria na taratibu simamizi
badala ya kuanza kujitangaza kwamba Zanzibar ni NCHI. Hata sisi wengine hapa
bara tunaona mabadiliko mengi yakifanyika kinyume lakini hatuwezi kuchukua
sheria mikononi kwani ikumbukwe tu kwamba Muungano wetu umetokana na WOGA
(fear) wa matukio kama haya.

Wapo wanaosema ilitokana na siasa kali za kina Abrahman Babu (communist) na
wengine wakidai hofu ya kurudi kwa Sultan kutokana na Mapinduzi yenyewe
kutokuwa na nguvu ya kutawala..Hivyo tunaporudia kuweka FEAR ndani ya mioyo
ya wananchi kugawanyika ili maslahi ya Zanzibar yawe mikononi mwa kundi
fulani, inarudisha hofu ileile iliyosababisha Muungano huu hivyo badala ya
kuuvunja huu Muungano ndio kwanza Hofu hii itaufanya Muungano kuwa imara
zaidi.

Kama alivyosema Mzee Mwanakijiji, kama kweli Wazanzibar hawautaki huu
Muungano basi ifanyike referendum (kura za maoni) hata iwe kwa Wazanzibar
peke yake. Hao viongozi kina Seif Sharrif na Karume wawaeleze wananchi FAIDA
na kujitenga na hasara za Muungano kwani ndiko kwenye kero. Na wawaeleze
Wazanzibar wakisha jitenga wao kama viongozi wataweza kufanya nini tofauti
ambacho wameshindwa kukitimiza wakiwa ndani ya serikali hii ya Muungano
maanke hjawa wote walikuwa viongozi wa ngazi ya juu ktk serikali hii.

Na unapotaka kuvunja ndoa zipo sheria na taratibu zake, sio rahisi kama
kuvua pete ya harusi na kuanza kutangaza Ukapera. Ndani ya refendum
Wazanzibar wataamua wanataka nini na hakika challenge hii nimeitoa kwa huyu
Seif, hao CUF na hata Baraza la Mapinduzi toka wakati Mkapa akiwa madarakani
lakini walishindwa kufanya hivyo wakisingizia mambo kibao. Maajabu ya Mussa
swala la serikali ya mseto, hizo kura za maoni zimepigwa haraka pasipo
kufikiria kero za Muungano sio jinsi ya kugawana madaraka baina ya viongozi
wa bara na visiwani.

Huu ni usaliti kwa wananchi wa Bara na Visiwani kwa sababu mfumo huu unazidi
kututenganisha zaidi tukifuata asili ya mtu kushika madaraka badala ya uwezo
wa mtu kushika madaraka na kibaya zaidi tunakimbia kero kubwa ya kiuchumi
ambayo hadi kesho serikali zote mbili zimeshindwa kuwa wazi kwa wananchi
kuhusiana na mgao wa pato la taifa. Badala ya hawa viongozi kuondoa kero za
Muungano ndiokwanza wameunda kero nyingine, viongozi wa vyama viwili
kukutana na kukubaliana ku share Madaraka ktk sehemu ya nchi ambayuo wao
wenyewe wanatutangazia kwamba sio Nchi wala Taifa. Na hata kama Zanzibar
ingekuwa Taifa ndani ya nchi bado hakuna nchi yoyote duniani inayotawaliwa
kwa mfumo unaotazama zaidi tamaa ya madaraka kwa viongozi zaidi ya
mustakabali wa nchi na raia wake.

CHANZO
[wanabidii] Marekebisho ya Katiba Zanzibar

0 comments:

Post a Comment