Wednesday, August 25, 2010

TAARIFA YA MKUTANO NA MHE DR SLAA

Wana FOS wote,

Kwanza niwaombe radhi kwa kuchukua muda mrefu sana katika kushughulikia suala la kufungua account. Tulichukua muda mrefu kwani kulikuwa na vikwazo kidogo. Ninayo furaha kuwafahamisha kuwa hatimaye tumeweza kupiga hatua muhimu na kufanikisha jambo muhimu sana la kufungua account kwa ajili ya michango ya kufanikisha ushindi wa Mh. Dr. Slaa.

Jina la account ni M4C
Account number ni: 01J108010100600
Benki ni CRDB.

Hivyo, karibuni sana katika kuwakilisha michango yenu kwa kadri ya uwezo wa kila mmoja wetu. Labda kuna mtu atapenda kufahamu kuwa M4C ni maana yake nini? Kwa kifupi maana yake ni Movement four Change.

Pili, napenda kuwafahamisha kuwa nimeongea na Mh. Dr. Slaa amenituma niseme kuwa anashukuru sana kwa moyo wenu na kwa uzalendo wenu mlioonyesha katika kumuunga mkono katika suala hili. Ameguswa sana na juhudi zetu hizi zimempa nguvu sana. Ametiwa moyo sana na hiki tunachojaribu kukifanya.

Kutoka na hilo basi, ametoa mualiko kwa wana FOS wote ili tuweze kukutana sote, tufahamiane, apate fursa ya kutushukuru, tuweze kubadilishana mawazo na muhimu zaidi tuweze kuwaeleza mipango ya FOS na pia kama mna maswali yoyote na michango basi mpate fursa ya kuuliza au kutoa michango yenu ya mawazo.

Hivyo basi, tunapendekeza kukutana siku ya Alhamisi. Muda, mahali na wakati tutafamishana baadae. Kwa sasa Mrs Slaa ambaye anamsaidia Mheshimiwa kuandaa mkutano huu, ameniomba niwasiliane nanyi na ku extend invitation hii kwenu na wale wote mtakaopenda kuhudhuria basi muwasiliane nami katika email yangu mki confirm kuhudhuria kwenu, ili name niweze kumfahamisha ni watu wangapi watakuja.

Nadhani hii ni fursa nzuri sana na ningewaomba tujitahidi kujipanga ili tuhudhurie.

Unaweza kuwasilina nami ku-confirm katika email yangu: srehani@hotmail.com au kwa simu 0756 20 96 66.

Pia nakaribisha mawazo yoyote yale ya kufanikisha mkutano huu muhimu. Kama una wazo usisite kunifahamisha. kuhusu program n.k.

Natanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu katika suala hili. Kwa sasa nahitaji kujua ni watu wangapi watahudhuria???

Asante

Selemani Rehani

NB: Unaweza kunipa namba yako ya simu na email address yako.

FUATILIA HABARI HIZI HAPA

FOS- Mkutano na Mh. Dr Slaa & Account Details

0 comments:

Post a Comment