Saturday, August 28, 2010

mtangazaji wa tbc1 nusura aipate joto ya jiwe jangwani

mtangazaji wa tbc1 nusura aipate joto ya jiwe jangwani

Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari wa usalama kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute nalo,wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio,hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa na jazba ya tukio hilo waliendelea kulalama mpaka Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe aliposimama na kuwasihii wananchi watulie na amani itawale eneo hilo la jangwani,na kweli baadae hali ikawa shwari na uzinduzi wa kampeni ukaendelea.
Baadhi ya askari wa usalama wakiwa wamemzonga Marin Hassan Marin wakijaribu kuweka sawa usalama wake katika eneo hilo,na baadaye yeye aliamriwa aondoke eneo hilo kwa usalama wake.
Mtangazaji wa shirika la Utangazaji la TBC1,Marin Hassan Marin akiombwa aingie kwenye gari na aondoke eneo la tukio kutokana na baadhi ya wanachi kutokufurahishwa na lill tukio la kukatishwa ghafla kwa matangazo hayo yaliyokuwa yakirushwa live na shirika hilo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,John Mnyika akiingilia kati kujaribu kuliweka sawa zogo hilo ambalo nusura liharibu hali ya hewa ya uwanjani hapo,pia kwa bahati nzuri vyombo vya usalama viliingilia kati na kujaribu kuweka hali shwari kwa wananchi waliokuwepo uwanjani hapo.
Pichani mmoja wa wananchi akionekana kung'aka kwa hasira na kuanza kumfokea mtangazaji wa TBC1,Marin Hassan Marin mara baada ya kubainika kukatizwa kurushwa kwa matangazo ghafla ya uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE kupitia shirika hilo jioni ya leo.
Katika hali isiyo ya Kawaida,Mpiga Picha na Mtangazaji mahiri wa shirika la Utangazaji la TBC1,Marin Hassan Marin walijikuta ndani ya wakati mgumu kwa baadhi ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo wakati wa uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama cha CHADEMA leo jioni,mara baada ya kubaini shirika la utangazaji la TBC1 kukatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kuleta fujo ya kutaka kuharibu mitamb0 ya Shirika hilo huku wakitishia kumpiga mtangazaji huyo.

0 comments:

Post a Comment