Tuesday, August 10, 2010

MRITHI WA SLAA KARATU APOKEWA


Mgombea wa ubunge kwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Karatu,mchungaji Israel Yohana Natse akihutubia umati wa wananchi wa mjini Karatu.Sehemu ya umati wa wananchi wa mjini Karatu wakimsikiliza mgombea wa Chadema katika jimbo la karatu mchungaji Israel Yohana Natse

Novatus Makunga,Karatu

Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani hapa wamemlaki kwa maandamano makubwa pamoja na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Karatu kumlaki mgombea wa ubunge wa chama hicho katika jimbo la hili ambalo limeachwa na katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa

Slaa aliyeamua kujitosa katika urais ameliongoza jimbo hilo tangu mwaka 1995 baada ya kujiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na jina lake kuenguliwa baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge kabla yake Patrick Qorro.

Mgombea huyo ambaye ni mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini (KKKT) katika jimbo la Karatu mchungaji Israel Yohana Natse alisema kuwa amejitosa katika ubunge ili kuitumikia jamii kwa upana zaidi.

Alisema kuwa kutokana na kushirikiana na mbunge anayemaliza muda wake Dk Slaa katika miradi mbalimbali amejipima na kubaini kwamba ana uwezo mkubwa na kuwaongoza wananchi wa Karatu.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba viatu alivyoviacha Slaa nina uwezo mkubwa wa kuvivaa pengine hata zaidi ya Slaa kwa kuwa miradi mingi tumeisimamia pamoja,"alisema mgombea huyo.

Alileeza kwamba kipaumbele kwake kitakuwa ni elimu kuanzi ya ngazi ya chini mpaka elimu ya juu na hasa mchakato ulioanza wa kuanzisha Chuo kikuu cha Karatu ambapo yeye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya chuo hicho.

Alisma kuwa Chuo hicho kitachukuwa majengo ya shule ya sekondari ya Karatu huku shule hiyo ikiamishiwa eneo la Ganako.

Aidha alisema kuwa ataendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha Chuo cha uuguzi na uganga kilichopo katika hospitali ya serikali wilayani Karatu ambacho pia ni mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa chuo hicho.

Katibu wa CHADEMA wilayani Karatu Laurent Bother alisema kuwa kuwa katika kumchagua mgombea huyo walizingatia uwezo wake katika kutekeleza katika ngazi ya jimbo na taifa yote yaliyoachwa na mtangulizi wake jimboni humo.

“Hata ukiangalia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza ni uthibitisho wa kwamba hali hii inaondoa dhana ya wapinzani wetu kwamba mikutano yetu inajaza watu kwa ajili ya helikopta

Alisema kwa chaguo hilo jimbo hilo kuchukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ni ndoto.

Awali wanachama wa chadema katika jimbo hilo walipinga vikali uamuzi wa Slaa kuacha jimbo na kwenda kugomba urais kabla ya yeye mwenyewe Dk Slaa pamoja na viongozi mbalimbali kwenda jimboni humo na kutoa ufafanuzi wa uamuzi wake huo

0 comments:

Post a Comment