Thursday, September 2, 2010

MAJIBU YA HOJA KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI 2003/04

MAJIBU YA HOJA KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI 2003/04

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwako wewe binafsi kwa kuongoza mjadala wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2003/04 kwa umahiri mkubwa. Aidha, napenda kutoa shukrani zangu kwa Naibu Spika, Mheshimiwa Juma J. Akukweti ambaye ameliongoza Bunge katika vikao kadhaa. Vile vile, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mhe. Anna Makinda pamoja na Mhe. Eliachim Simpasa ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa Wenyeviti wa vikao kadhaa vya mjadala huu pasipo kutetereka. Napenda nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi kwa kuwasilisha kwa ufasaha maoni ya Kamati yake. Napenda pia kumshukuru Mhe. Willbrod Slaa kwa mchango wake aliotoa kwa niaba ya kambi ya Upinzani.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wengi wamechangia mjadala huu kwa kuzungumza na wengine wamechangia kwa maandishi. Napenda nilihakikishie Bunge lako Tukufu kuwa Serikali inathamini sana michango ya Waheshimiwa Wabunge na inaichukua kama nyenzo muhimu ya kuboresha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Waheshimiwa Wabunge 80 wafuatao walipata fursa ya kuchangia mjadala kwa kuzungumza ndani ya Bunge:-

ORODHA YA WACHANGIAJI KWA KUZUNGUMZA

1. Mhe. Njelu E.M. Kasaka(Mb.) - Lupa

2. Mhe. Dr. Wilbroad P. Slaa (Mb.)- Karatu

3. Mhe. William Kusila(Mb.) - Bahi

4. Mhe. Prof.Simoni M. Mbilinyi(Mb.) -Peramiho

5. Mhe. Lucas L. Seleli (Mb.) - Nzega

6. Mhe. Dr. Diodorus B. Kamala (Mb.) - Nkenge

7. Mhe. Athumani S.M. Janguo (Mb.) - Kisarawe

8. Mhe. Mgana I. Msindai (Mb.) – Iramba Mashariki

9. Mhe. Jenista J. Mhagama(Mb.)- Viti Maalum

10 Mhe. Ireneus N. Ngwatura(Mb.) - Mbinga Mashariki

11.Mhe. Lekule M. Laizer (Mb.) - Longido

12.Mhe. Ponsiano D. Nyami (Mb.) - Nkasi

13.Mhe. Jackson M. Makweta(Mb.) - Njombe Kaskzini

14. Mhe. Edson Mbeyela Halinga(Mb.) – Mbozi Mashariki

15. Mhe. Balozi Getrudi I. Mongela (Mb.) - Ukerewe

16. Mhe. Ramadhan Khalfan(Mb.) - Bagamoyo

17. Mhe. Dr. Milton Makongoro Mahanga(Mb.) - Ukonga

18. Mhe. Henry D. Shekiffu (Mb.) - Lushoto

19. Mhe. Yete S. Mwalyego(Mb.) - Mbeya Vijijini

20. Mhe. Raphael Mlolwa(Mb.) - Kahama

21. Mhe. Beatus R. Magayane(Mb.) - Buyungu

22. Mhe. Suleiman A. Sadiq(Mb.) - Morogoro Kaskazini

23. Mhe. Magreth Mbwana(Mb.) - Viti Maalum

24. Mhe. John L. Mwakipesile(Mb.) - Kyela

25. Mhe. Philip Marmo(Mb.) - Mbulu

26. Mhe. Charles Kagonji(Mb.) - Mlalo

27. Mhe. Damas Nakei(Mb.) – Babati Magharibi

28. Mhe. Rudovick Mwananzila(Mb.) - Kalambo

29. Mhe. Isaac Cheyo(Mb.) - Bariadi Magharibi

30. Mhe. Fatma Said Ally(Mb.) - Mlandege

31. Mhe. Aggrey Mwanri(Mb.) - Siha

32. Mhe. Anna Makinda(Mb.) - Njombe Kusini

33. Mhe. Omari Kwaangw’,(Mb.) - Babati Mashariki

34. Mhe. John E. Singo(Mb.) - Same Magharibi

35. Mhe. Ernest G. Mabina(Mb.) - Geita

36. Mhe. Christopher Wegga(Mb.) - Mikumi

37. Mhe. Eliachim Simpasa(Mb.) - Mbozi Magharibi

38. Mhe.Capt. Theodos Kasapila(Mb.) - Ulanga Mashariki

39. Mhe. Abdula Lutavi(Mb.) - Tandahimba

40. Mhe.Aisha Kigoda(Mb.)-Viti Maalum

42. Mhe. Hassan R. Khatib(Mb.) - Amani

43. Mhe. Mariam S. Mfaki(Mb.) - Viti Maalum

44. Mhe. Nimrod E. Mkono(Mb.) - Musoma Vijijini

45. Mhe. Dr.Thadeus Luoga(Mb.) - Mbinga Magharibi

46. Mhe. Raymond Mrope(Mb.) - Masasi

47. Mhe. William Shelukindo(Mb.) - Bumbuli

48. Mhe.Mwanne Mchemba(Mb.) - Viti Maalum

49. Mhe. Mohamed R. Soud(Mb.) - Jang’ombe

50. Mhe.Thomas Ngawaiya(Mb.) - Moshi Vijijini

51. Mhe. Prof. J. Maghembe(Mb.) - Mwanga

52. Mhe.Eshterina Kilasi(Mb.) - Mbarali

53. Mhe.Paul Ntwina(Mb.) - Songwe

54. Mhe.A. Karavina(Mb.) - Urambo Mashariki

55. Mhe.Joel Bendera(Mb.) - Korogwe Mashariki

56. Mhe. James M. Musalika(Mb.) – Nyang’wale

57. Mhe. Nazir Karamagi(Mb.)- Bukoba Vijijini

58. Mhe. Kidawa Saleh(Mb.) - Viti Maalum

59. Mhe.Kilontsi Mporogomyi(Mb.) - Kasulu Magharibi

60. Mhe. Issa M. Suleimani(Mb.) - Magomeni

61. Mhe. Herbet Mntangi(Mb.) - Muheza

62. Mhe. Omar Nguli(Mb.)-Singida Mjini

63. Mhe. Omar Mloka - Morogoro Mjini

64. Mhe.Semindu Pawa(Mb.)-Morogoro Kusini Mashariki

65. Mhe.Juma S. Kidunda(Mb.)-Kilindi

66. Mhe.Mwanamkuu Kombo(Mb.)-Viti Maalum

67. Mhe.Monica N. Mbega N. Iringa Mjini

68. Mhe.Venance M. Mwamoto (Mb.)Kilolo

69. Mhe.Benito Malangalila(Mb.)-Mufindi Kusini

70. Mhe.Abu T.Kiwanga(Mb.) –Kilombero

71. Mhe.Ali S. Salim(Mb.)-Ziwani

72. Mhe.Benson M. Mpesya(Mb.) – Mbeya Mjini

73. Mhe.Mbaruk Mwandoro(Mb)-Mkinga

74. Mhe. Aridi M.Uledi(Mb.)-Masasi

75. Mhe.Ester Nyawazwa(Mb.)-Mwanza

76. Mhe. Emmanuel E. Kipole(Mb.)-Msalala

77. Mhe.Talala Mbise(Mb.)-Arumeru Mashariki

78. Mhe. Prof. Daimon M. Mwaga(Mb.)-Kibakwe

79. Mhe.Frank G. Magoba(Mb.)-Kigamboni

80. Mhe. Zahoro Juma Khamis(Mb.)-Chumbani

Hali kadhalika, katika mjadala huu, Waheshimiwa Wabunge 54 wafuatao walichangia kwa maandishi:-

ORODHA YA WACHANGIAJI KWA MAANDISHI

1.Mhe. Alhaj. Shaweji Abdallah(Mb.) - Kilosa

2. Mhe. Prof. Henry R. Mgombelo (Mb.) - Tabora Mjini

3. Mhe. Frank Michael Mussati (Mb.) - Kasulu Mashariki

4. Mhe. Mgana Msindai(Mb.) – Iramba Mashariki

5. Mhe. Mohamed A. Abdulaziz(Mb.) - Lindi Mjini

6. Mhe. Dr. Milton M. Mahanga (Mb.) - Ukonga

7. Mhe. Ruth Blasio Msafiri(Mb.) - Muleba Kaskazini

8. Mhe. Parmukh Singh Hoogan(Mb.) - Kikwajuni

9. Mhe. Anatory K. Choya(Mb.) - Biharamulo Magharibi

10.Mhe.Shamim Khan(Mb.) - Viti Maalum

11.Mhe. Leonard Derefa(Mb.) - Shinyanga Mjini

12.Mhe. Mhe. Magareth Mkanga(Mb.) - Viti Maalum

13.Mhe. Major Jesse J. Makundi(Mb.) – Vunjo

14.Mhe. Kheri K. Ameir(Mb.) - Matemwe

15.Mhe. Mwadini Abass Jecha(Mb.) - Utaani

16.Mhe. Mwanaidi Hassan Makame (Mb.) - Kuteuliwa

17.Mhe. Fatma S. Ali(Mb.) - Mlandege

18.Mhe. Job Y. Ndugai(Mb.) - Kongwa

19.Mhe. Tembe K. Nyaburi(Mb.) - Bunda

20.Mhe. Diana Mkumbo Chilolo(Mb.) - Viti Maalum

21.Mhe. Sijamini Mohamed Shaame (Mb.) - Kitope

22.Mhe. Rhoda L. Kahatano(Mb.) - Viti Maalum

23.Mhe. Mbaruk K. Mwandoro(Mb.) - Mkinga

24.Mhe. Halimenshi Mayonga(Mb.) - Kigoma Kaskazini

25.Mhe. Remidius E. Kisassi(Mb.) - Dimani

26.Mhe. Stanley H. Kolimba(Mb.) - Ludewa

27.Mhe. Mossy Suleimani Mussa(Mb.) - Mfenesini

28.Mhe. Peter Kabisa(Mb.) - Kinondoni

29.Mhe. Mohamed Rished Abdallah(Mb.) - Pangani

30.Mhe. Jacob D. Shibiliti(Mb.) - Misungwi

31.Mhe. Prof. Mark Mwandosya(Mb.) - Rungwe Mashariki

32.Mhe. Anna Abdallah(Mb.) - Lulindi

33.Mhe. Omari S.L. Chubi (Mb.) - Kilwa Kaskazini

34.Mhe. Khalid Suru(Mb.) - Kondoa Kaskazini

35.Mhe. Antony M. Diallo(Mb.) Mwanza Vijijini

36.Mhe. Zakia Hamdani Meghji-Viti Maalum

37.Mhe. Hadija Kusola Kusaga (Mb.) Temeke

38.Mhe. Samuel M. Chitalilo(Mb.)-Buchosa

39.Mhe. Shaib Ameir(Mb.)Mwembe Makumbi

40.Mhe. Major Jesse J. Makumbi (Mb.) –Vunjo

41.Mhe. Dr. Maua A. Daftari(Mb.) Viti Maalum

42.Mhe. Mohamed Suleiman(Mb.)-Magomeni

43.Mhe. Elizabeth N. Batenga(Mb.)-Viti Maalum

44.Mhe. Dr. Wilbroad Slaa(Mb.)- Karatu

45.Mhe. Ally Machano Musa (Mb.) – Tumbatu

46. Mhe. Ussi Yahya Haji (Mb.) - Chaani

47. Mhe. Mohamed Rajabu Soud (Mb.) – Jang’ombe

48. Mhe. Damas Pachal Nakei (Mb.) – Babati Magharibi

49. Mhe. Esha H. Stima (Mb.) – Viti Maalum

50. Mhe. Shaibu Ahmada Ameir (Mb.) – Mwembe Makumbi

51. Mhe. Dr. Lucy S. Nkya (Mb.) – Viti Maalum

52. Mhe. Bahati Ali Abeid (Mb) – Viti Maalum

53. Mhe. Kijakazi Khamis Ali (Mb.) – Viti Maalum

54. Mhe. Semindu K. Pawa (Mb.) – Morogoro Kusini Mashariki

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema hapo awali, Serikali inathamini na kuheshimu michango ya Waheshimiwa Wabunge wote. Manaibu Waziri wa Fedha Mhe. Abdisalaam Issa Khatibu (Mb.) na Mhe. Dr. Festus Limbu (Mb.) leo asubuhi walitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge. Namshukuru pia Mhe. Abdallah Kigoda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji; kwa maelezo yake leo asubuhi kuhusu michango ya Wabunge. Kwa kuzingatia kwamba Wabunge 134 walichangia mjadala wa Bajeti hii, sio rahisi kwetu sisi kujibu au kutoa maelezo na ufafanuzi wa kila hoja ya Mheshimiwa Mbunge siku ya leo. Ninachoweza kuahidi ni kwamba hoja zote zitafanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha sera na utendaji wa Serikali kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kusema hayo napenda na mimi nitoe maelezo machache kuhusu baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-

MGAO WA FEDHA KISEKTA NA KIMKOA

Mheshimiwa Spika, baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walizungumzia suala bajeti Kisekta na Kimkoa. Bajeti ya Serikali ina sehemu kubwa mbili ambazo ni Mapato na Matumizi. Sehemu ya mapato ni ngumu zaidi kuliko matumizi na hivyo bajeti yoyote ile hutegemea sana mapato yake.

Kwa hiyo vigezo vinavyotumika katika kugawa fedha za bajeti kitaifa ni pamoja na:-

(i) Mapato ya ndani, misaada na mikopo kutoka nje;

(ii) Mahitaji ya Deni la Taifa. Hili ni ‘first charge’ kwa mujibu wa Sheria ya Fedha;

(iii) Mahitaji ya mishahara ya watumishi wa Serikali na Taasisi zake. Fedha za mishahara hutengwa kulingana na watumishi waliopo katika kila Wizara, Mkoa na Halmashauri. Mishahara nayo ni (first charge)

(iv) Mahitaji ya sekta za kuondoa umaskini. Sekta za kuondoa umaskini kama zilivyoainishwa kwenye Mkakati wa Kuondoa Umaskini zinapewa kipaumbele katika mgao wa fedha kuliko zingine. Sekta zinazohusika ni pamoja na Afya, Elimu, Maji, Kilimo, Mahakama, Barabara na mapambano dhidi ya UKIMWI.

(v) Mahitaji ya ulinzi na usalama yamepewa kipaumbele katika bajeti hii. Vyombo vinavyohusika ni Polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi, Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Mambo ya Nje.

vi) Mihadi ya Serikali. Pale ambapo kuna mihadi ya Serikali, hupewa kipaumbele, kuhakikisha kuwa Serikali inatimiza ahadi zake na kuendeleza shughuli zilizokwisha anzishwa;

MGAWANYO WA MATUMIZI KIMKOA

Kwa upande wa Mikoa na Halmashauri za Wilaya, vigezo ambavyo hutumika ni pamoja na wingi wa shule, idadi ya wanafunzi, zahanati, vituo vya afya, urefu wa barabara na wa miundombinu iliyopo kwa ujumla.

Kwa mwaka 2003/04, mgao wa fedha zetu wenyewe (local) za maendeleo kwa mikoa pamoja na mambo mengine, umezingatia mambo yafuatayo:

i) Miradi inayoendelea.

ii) Uanzishaji wa Wilaya /Miji mipya ambayo inahitaji nyumba za watumishi na maboma.

iii) Mikoa ambayo haina fedha za nje imeongezewa fedha za ndani. Mikoa inayohusika na nyongeza hii ni DSM, Rukwa, Kigoma, Tabora, Shinyanga, na Dodoma.

iv) Mkoa wa Manyara umetengewa fedha kwa ujenzi wa Boma na nyumba ya Mkuu wa Mkoa.

Mikoa ambayo inaonekana ina fedha nyingi za ndani, licha ya kuwa na fedha za nje, ni kwa sababu ama ina Wilaya mpya au miradi inayoendelea ambayo inahitaji mchango wa Serikali (counterpart funds).

Mheshimiwa Spika, ni vyema ikumbukwe kwamba kuna misaada ya fedha na mali ambayo inapelekwa moja kwa moja mikoani na ambayo haionyweshi kwenye bajeti. Kwa mfano:-

MKOA WA KIGOMA

i) Mwandiga – Manyovu Road Rehabilitation Shs. 478.2 milioni

ii) District Development Programme Euro 3,000,000 belgium

iii) Kigoma Micro Project (EU) 473.3 milioni.

iv) Lake Tanganyika (catchments EU) shs. 323.2 milioni.

MKOA WA SHINYANGA

i) Sustainable Rural Water Supply Euro 7m Netherland

ii) Community Based Organization 30.0 m

iii) Sukumaland Food Security (Australia) A$241,440

iv) Water Development (TAWASA) A.$241,440

MKOA WA TABORA

i) Integrated Pest management – 419.6m Germany

ii) Rural Electrification – Urambo District – SEK 50.0m SIDA

iii) Environment (Conservation) USAID 203.1 mln

MKOA WA RUKWA

i) Energy Efficiency and Conversation Shs. 1.36 KFW

ii) Rehabilitation of Health Units in Mpanda District Tshs. 91.9 mln Japan

MISAADA NA MIKOPO KUTOKA NCHI ZA NJE

Kwa upande wa miradi ya maendeleo, Wahisani wamekuwa na upendeleo katika sekta fulani na baadhi ya maeneo. Hili ni suala la kihistoria, lakini Serikali imechukuwa hatua kurekebisha mwenendo huu. Serikali imetoa mwongozo (Tanzania Assistance Strategy) wa jinsi ya kusimamia misaada kutoka nchi za nje. Mwongozo huu unatoa mamlaka kwa Serikali kuchagua ‘priority’ ambazo zitaingia katika mipango na bajeti ya Serikali na wahisani wanapaswa kuelekeza misaada yao kwenye maeneo hayo. Wafadhili wote wanaunga mkono mwongozo huu na wengi sasa wanatoa sehemu kubwa ya misaada na mikopo yao kupitia programu za sekta (Sector Wide au Programme Approach) au moja kwa moja kwenye bajeti (Direct Budget Support). Hatua hii imepunguza kwa kiwango fulani tatizo la wahisani kuchagua mradi au mkoa fulani (Donor Driven Assistance). (kwa mfano, misaada na mikopo kupitia ‘Sector Wide Approach’/Basket Fund’ imeongezeka kutoka shillingi 27,011 milioni mwaka 2001/2002 hadi shillingi 58,252 milioni robo ya tatu ya mwaka 2002/03 na inatarajiwa kufikia shilingi 191,182 milioni kwa mwaka 2003/04. ‘Budget Support’ imeongezeka kutoka shilingi 172,823 milioni mwaka 2001/02 hadi shilingi 182,614 milioni robo ya tatu ya mwaka 2002/03 na inatarajiwa kufikia shilingi 405,047 milioni kwa mwaka 2003/04) Hata hivyo, kuna miradi michache ambayo inaendelea kwa misingi ya zamani kutokana na sababu za mihadi ya mikataba, na ukweli kwamba, kuna wafadhili wachache ambao hawataki kubadili taratibu zao za kutoa misaada.

Kutokana na mabadiliko hayo kutoka ‘Project Type Assistance’ na kwenda kwenye ‘Sector Wide Programme’, na ‘Direct Budget Support’, sehemu kubwa ya misaada na mikopo sasa inagawiwa mikoani kupitia njia zifuatazo:-

i. Moja kwa moja kwa bajeti ya matumizi ya kawaida (OC).

ii. Miradi/programu za kitaifa zinazotekelezwa chini ya Mkakati wa Kuondoa Umaskini. Kwa mfano, mradi wa PEDP, programu ya kurekebisha sekta ya afya (Health Sector Reform Program), Mkakati wa kupambana na UKIMWI, barabara n.k.

UDHIBITI WA BAJETI

Mheshimiwa Spika, Usimamizi na utekelezaji wa bajeti ni muhimu sana ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanapatikana. Mpaka sasa Serikali imeendelea kuimarisha na kuboresha utaratibu wake wa kutenga fedha, ambao unalenga kwenye matokeo (performance budget). Chini ya utaratibu huu kila Wizara, Idara na Mkoa, huainisha malengo (targets) za kutekeleza katika bajeti za kila mwaka pamoja na kuangalia kazi iliyotekelezwa (value for money).

Ratiba za utekelezaji (action plans) na mtiririko wa fedha (cash flow plans) kwa kila Wizara, Mkoa na Wilaya zinaandaliwa ili zitumike katika kufuatilia utekelezaji wa bajeti ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo.

Hivyo, kwa kufuatilia na kukagua matumizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mara kwa mara, tutaweza kubaini matatizo mapema na kuchukua hatua zinazostahili. Pale fedha za nje zinapohusika tunawahimiza wafadhili walete fedha kwa wakati.

Aidha, udhibiti wa matumizi kwa mtandao wa IFMS nao unaimarishwa ili kupata taarifa sahihi za mapato na matumizi kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, katika eneo hili la usimamizi na udhibiti wa bajeti, nawaomba Waheshimiwa Wabunge washirikiane na Serikali kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha na utekelezaji wa miradi ya maendeleo yanafanyika katika maeneo yenu kama ilivyopangwa.

HOJA YA KWAMBA CASH BUDGETING INAATHIRI UTEKELEZAJI WA BAJETI NA HASA MIRADI YA MAENDELEO

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa ‘cash budgeting’ ulianzishwa kutokana na mwenendo wa matumizi ambao haukuwa unaendana na mapato halisi. Tangu Serikali ianze kutumia utaratibu huu, matumizi ya Serikali kwa kiwango kikubwa yamedhibitiwa na sasa tunatumia kulingana na mapato yetu, na hii imesaidia sana kutufikisha kwenye uchumi tulivu (macroeconomic stability) na katika kujenga nidhamu ndani ya Serikali. Hata hivyo, utaratibu wa ‘cash budget’ unarekebishwa kadri tunavyopata uzoefu. Sekta za kuondoa umaskini zinapewa fedha zao kwa miezi mitatu mitatu, na utekelezaji wa miradi ya sekta hizo haukwamishwi na ‘cash budget’ hata kidogo.

Tunaendelea kuchukua hatua za kuboresha utaratibu wa ‘cash budgeting’ kwa kuzingatia mwenendo wa kukusanya mapato pamoja na usimamizi wa matumizi

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi ya maendeleo umekuwa chini ya malengo kutokana na sababu zifuatazo: -

i) Ufahamu mdogo wa sheria ya ununuzi uliosababisha ucheleweshaji wa miradi inayotekelezwa na makandarasi au miradi yenye manunuzi makubwa. Hata hivyo, sheria ya ununuzi inachambuliwa upya na italetwa Bungeni kwa marekebisho.

ii) Sababu nyingine ni kwamba fedha za miradi kutoka nje ambazo zinahusu vifaa na huduma (direct to project funds) haziingizwi kikamilifu katika hesabu za Serikali. Kwa hiyo, japokuwa katika para 25 ya hotuba yangu nilisema kwamba matumizi ya fedha za maendeleo kwa miezi tisa yaani Julai, 2002 hadi Machi, 2003 yalikuwa asilimia 56.2 tu, upo uwezekano mkubwa kwamba sehemu kubwa ya misaada kutoka kwa wahisani imeshatolewa. Aidha, katika kipindi cha mwisho, matumizi yanaweza kufikia kiwango kilichotengwa kwenye bajeti, kwa kuwa takwimu kutoka kwenye miradi sasa zinakuja kwa kasi kubwa.

RUZUKU YA PEMBEJEO

Mheshimiwa Spika, Ruzuku ya pembejeo za Kilimo ambayo Serikali inaanzisha katika bajeti hii ina lengo la kuimarisha uzalishaji kwa kuongeza tija katika Kilimo cha Mazao ya chakula na biashara. Mkazo wa kwanza kwa mwaka wa fedha ujao wa 2003/04 utakuwa chakula.

Mpango huu ambao ndio tunaanza kuutekeleza utasaidia kujifunza mambo mengi. Hivyo, mafanikio yatakayojitokeza yatawezesha Serikali kuamua iwapo utaratibu huu utakuwa wa kudumu au la. Jambo la msingi na changamoto kwetu kama Waheshimiwa Wabunge ni kusimamia kwa dhati matumizi ya pembejeo zitakazohusika katika maeneo yenu ili mpango huu, ufikie malengo yaliyokusudiwa. Serikali chini ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo na Chakula itaandaa utaratibu utakaofaa wa kutekeleza mpango huu.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna haja ya kuwa na Benki ya kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa sekta za Kilimo, Viwanda na Miundo Mbinu. Serikali inadhamiria kuanzisha benki ya aina hii na kwa kuanzia Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia TIB kwa madhumuni haya. Mheshimiwa Spika, mahitaji ya mikopo midogo (microfinance) kwa miradi midogo na biashara ndogo ndogo ni tofauti na yale ya mikopo ya muda wa kati na mrefu.

Kwa hiyo NMB itaendelezwa kwa madhumuni ya kutoa mikopo midogo midogo (microfinance lending) kama ilivyokuwa imekusudiwa.

MADUKA YA FEDHA ZA KIGENI

Mheshimiwa Spika, biashara ya maduka ya fedha za kigeni (Bureau de change) inaongozwa na sheria ya fedha za kigeni (Foreign Exchange Act, 1992) na kanuni (Regulations) zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania chini ya sheria hiyo. Kanuni hizo zinaelekeza wazi jinsi maduka haya yanavyopaswa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kutoa risiti za mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni, kuweka bango ndani ya kila duka linalomtaka kila mteja kupewa risiti kwa ajili ya mauzo au manunuzi yaliyofanyika na kuweka bango linaloonyesha bei ya kununua na kuuza fedha za kigeni.

Pia, miongozo hii inaainisha kuwa biashara ya maduka haya ni ya papo kwa papo (spot transaction). Maduka hayo yanatakiwa kuwasilisha Benki Kuu ripoti za kila mwezi kuhusu mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni, risiti za mauzo na manunuzi ya bei (exchange rates) za kuuza na kununua fedha za kigeni. Benki Kuu kwa upande wake inafanya uchambuzi wa taarifa hizi ili kufahamu hali halisi ya biashara ya kila duka. Aidha, Benki Kuu hufanya ukaguzi (on – site examination) kila duka mara moja kwa mwaka, na wakati mwingine hufanya ukaguzi wa dharura (surprise checks) pindi kunapokuwa na taarifa zinazoashiria kuwa duka husika linaendesha biashara bila kufuata kanuni iliyowekwa.

MIPANGO YA KILIMO WILAYANI

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mpango wa maendeleo ya kilimo wilayani, Serikali imeamua kutenga fedha kwa ajili hiyo katika bajeti ya 2003/04. Fedha zilizotengwa zitatumika katika kuendeleza zao moja la biashara na moja la chakula kwa kila Wilaya. Kutokana na tofauti zilizopo katika wilaya na hata kata, ni jukumu la viongozi na wananchi wa wilaya husika kuchagua mazao mawili ili tuweze kupata uzoefu wa kuonyesha matokeo ya fedha walizopokea ili kupata ‘value for money’. Waziri wa Kilimo na Chakula na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, watasimamia utekelezaji wa mpango huu.

FEDHA ZA STABEX

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa inapata fedha za Stabex kwa muda mrefu kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya chini ya “ACP/EU Framework”. Kwa kawaida fedha hizi zilikuwa zinatumika kutoa fidia kwa wakulima wa kahawa kupitia Vyama vya Ushirika ambavyo vilikuwa vinanunua kahawa ya wakulima na kuweka kumbukumbu vizuri.

Matumizi mengine ya Stabex kwa siku za nyuma yalikuwa:-

· Kuimarisha barabara za kahawa

· Kuimarisha ubora wa kahawa, na kuendeleza

· Utafiti wa zao la kahawa

Baada ya kupata taarifa kuhusu fedha mpya za Stabex tuliwasiliana na EU na kupendekeza fedha zitumike kama ilivyofanyika siku za nyuma i.e.

i. Fidia kwa wakulima wa kahawa Euro 17 m

ii. Kuimarisha barabara za kahawa Euro 8 m

iii. Kuimarisha ubora wa kahawa Euro 5.4 m

iv. Utafiti wa zao la kahawa Euro 3 m

Hata hivyo baada ya majadiliano ya muda mrefu ilishindikana kukubaliana fedha hizi kutumika kama Serikali ilivyotarajia kwa sababu zifuatazo:-

i. Haikuwa rahisi kupata takwimu za uhakika zinazoonyesha mauzo ya kila mkulima. Hali hii inatokana na soko huria lililoanzishwa nchini kabla ya mwaka 1999.

ii. Kutokana na tatizo la takwimu kulikuwa na uwezekano mkubwa wa fedha hizi kutumiwa na wasio walengwa na hivyo kupoteza maana.

Kwa kuzingatia sababu hizi, na ili kuhakikisha kuwa Serikali haipotezi fedha hizi, tulikubaliana matumizi yake yalenge katika mkakati wetu wa kuendeleza kilimo (ASDP) na kuzingatia tathmini ya matumizi ya mpango wa Stabex uliopita (Stabex 1992/93).

Hivyo, baada ya majadiliano ya muda mrefu, Serikali ililazimika kukubaliana na EU kwamba fedha za Stabex (Kahawa) za mwaka 1994/99 - Euro 38 milioni sawa na Tsh. 42 bilioni zitumike kama ifuatavyo:-

i. Kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP) - Euro 18.0 milioni. Wizara ya Kilimo na Chakula inasimamia suala hili.

ii. Ukarabati wa barabara muhimu za mikoa inayozalisha kahawa – Euro 10 milioni. Suala hili linashirikisha Wizara za Ujenzi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; TANROADS na Road Fund.

iii. Utafiti wa kahawa pamoja na “extension services” – Euro 9.0 milioni.

iv. Euro 1.0 milioni zitatumika kwa ajili ya ukaguzi, ushauri wa kitaalamu na tathmini nzima ya utekelezaji wa programu nzima ya Stabex.

Mwisho, Mkataba kuhusu matumizi ya fedha hizi ulisainiwa kati ya Serikali na Jumuiya ya Nchi za Ulaya mwezi Februari mwaka huu na kutangazwa katika vyombo vya habari.

KUANZISHWA KWA UNIT TRUST OF TANZANIA (UTT).

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Privatization Trust ya mwaka 1997, muda wa Privatization Trust (PT) ulimalizika tarehe 15 Juni, 2003. Aidha, Sheria hiyo ilitamka bayana kwamba muda wa PT utakapomalizika, chombo hiki kinaweza kujibadili na kuwa Unit Trust. Kwa kuzingatia uamuzi wa Serikali wa kuanzisha Unit Trust of Tanzania (UTT) kwa njia hii, Bodi ya Wadhamini wa UTT iliteuliwa tarehe 7 Juni, 2003 na muda wao wa kuanza kazi ulikuwa tarehe 16 Juni, 2003. Hivyo, kufuatia kumalizika kwa muda wa PT tarehe 15 Juni 2003, PT “automatically” ilijigeuza kuwa Unit Trust of Tanzania ilipofika tarehe 16 Juni 2003.

Mheshimiwa Spika, kufuatia hatua hiyo, Bodi ya Wadhamini wa UTT ilikutana tarehe 17 Juni 2003 na kuidhinisha Trust Deed ambayo ilikuwa imeandaliwa. Baada ya Wadhamini wote kusaini Trust Deed, UTT imeandikishwa rasmi na Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali. Mheshimiwa Spika, naomba samahani kama maandishi katika hotuba yangu ya bajeti kuhusu jambo hili hayakueleweka vizuri.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa dhana ya uwekezaji mdogo (collective investment schemes) ni ngeni miongoni mwa Watanzania wengi, suala la elimu kwa umma ni muhimu sana. Wakati wa PT muda mwingi ulitumika kujifunza na kuelimisha. UTT kwa kushirikiana na CMSA kama msimamizi wa shughuli za UTT, itatoa elimu kwa Umma katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika vizuri. Aidha, hisa asilimia 10 za Kampuni ya Bia (TBL) na asilimia 3 za Kampuni ya Sigara (TCC) zilizotolewa kama “seed capital” ya kuanzisha UTT sasa zitaanza kuelekezwa kwa Wananchi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Marmo katika mchango wake kwenye Hotuba ya Bajeti ya 2003/04 aliuliza maswali yafuatayo:

i) Nini wajibu wa Benki Kuu katika kusimamia Benki za Biashara?

ii) Kwa nini Gavana hawajibishwi kwa benki zinazoanguka, kama Benki ya Delphis?

iii) Kwa nini Benki Kuu inaruhusu Wakurugenzi na wawekezaji wabaya kwenye Benki za Biashara kama Somaia wa Benki ya Delphis?

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Marmo kama ifuatavyo:-

i) Wajibu wa usimamizi wa shughuli zote za mabenki na taasisi za fedha hapa nchini upo chini ya Benki Kuu ya Tanzania. Wajibu huo unahusu kuhakikisha kuwa benki za biashara na taasisi za fedha zinafanya kazi zake kulingana na sheria ya mabenki na miongozo iliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Wajibu huo unahusisha utoaji wa leseni kwa benki na taasisi hizo na usimamizi wa shughuli za vyombo hivyo.

Wajibu na majukumu haya ya Benki Kuu ya Tanzania juu ya usimamizi wa benki za biashara na taasisi za fedha umeainishwa katika sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 1991 (Banking and Financial Institutions Act, 1991) na sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 1995 (Bank of Tanzania (BoT) Act , 1995). Kulingana na sheria hizo mbili wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania kusimamia benki za biashara na taasisi za fedha unajumuisha shughuli zifuatazo:-

a) Utoaji wa leseni kwa benki za biashara na taasisi za fedha zinazoomba kuendesha shughuli zao hapa chini.

b) Usimamizi wa benki za biashara na taasisi za fedha zilizopewa leseni; kuhakikisha kwamba vyombo hivi vinaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria. Usimamizi huu unahusisha ukaguzi wa shughuli za kila benki hapa nchni (On site Examination) na pia uangalizi na ufuatiliaji wa shughuli za kila benki kwa kutumia ripoti ambazo mabenki na taasisi za fedha zinawasilisha Benki Kuu ya Tanzania (Offsite Supervision).

Ukaguzi na ufuatiliaji wa mienendo ya benki za biashara na taasisi za fedha unafanywa kwa lengo la kuhakikisha kuwa benki hizo zinakuwa na mtaji wa kutosha, rasilimali nzuri (good assets), wawekezaji na menejimenti wanaofaa, zinapata faida, na hazifanyi shughuli zisizoruhusiwa na sheria (prohibited activities); na kwa ujumla zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

c) Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania juu ya vyombo hivi vya fedha ni pamoja na kutoa miongozo, taratibu, makaripio, adhabu kwa vyombo husika na kwa wenye hisa na menejimenti za taasisi hizo, kwa mujibu wa sheria.

ii) Mheshimiwa Spika, napenda ieleweke kuwa wajibu wa Benki Kuu katika kusimamia biashara ya kibenki (banking business) ni kuhakikisha kuwa katika biashara hii kuna uhuru wa kuingia na kufanya biashara kwa mujibu wa sheria na miongozo na pia pale ambapo benki imeshindwa kufanya kazi zake kwa faida na kwa mujibu wa sheria basi ichukuliwe hatua na ikibidi ifungwe na iondolewe katika biashara hiyo kwa utaratibu unaokubalika (Orderly Entry and Exit). Kuanguka kwa benki ni jambo ambalo linajulikana na sababu ni zile zile zinazoifanya kampuni yoyote nyingine ianguke. Kwa upande wa Tanzania, sababu kubwa ya benki kuanguka au kupata matatizo imekuwa kwanza ukosefu wa uaminifu kwa wale wenye benki. Na hicho ni kitu ambacho binadamu yeyote hawezi kutambua kwa sababu mwenye benki anaweza kuwa na uaminifu na akajulikana kuwa ni raia mzuri sana kwa miaka mingi. Lakini siku moja huenda ikatokea akaivamia benki yake mwenyewe na kutoroka na pesa za wateja. Sababu ya pili inayosababisha benki kuanguka ni kutorejeshwa kwa fedha zilizokopwa. Kwani tukumbuke kuwa benki hazina fedha, ila fedha zinazokopeshwa na benki zinatokana na amana (deposits) za wateja. Kwa hiyo wakopaji wakishindwa kulipa benki inakuwa haina njia ya kuwarudishia wateja amana (deposits) zao hapo watakapozitaka. Na kwa sababu ya kushindwa kulipa wateja amana (deposit) zao benki inaanguka. Hata hivyo, kwa bahati nzuri jambo hilo ni nadra kutokea hapa kwetu kwa sababu kabla benki haijazorota, Benki Kuu huingia na kuitwaa hiyo benki na kuiweka chini ya uongozi wake.

Kwa kifupi, kama biashara nyingine zozote katika uchumi wa nchi zinavyotetereka na kuanguka, benki pia zinatetereka na kuanguka kutokana na sababu mbalimbali kama vile mazingira mabaya ya kibiashara, ukosefu wa mitaji, kupata hasara kwa upungufu wa uaminifu wa menejiment au watendaji wenye dhamana ya uendeshaji wa siku hadi siku wa taasisi hizo na kwa sababu nyingine mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo maelezo hapo juu utaona kuwa Benki Kuu ya Tanzania haiwezi kuzuia moja kwa moja uangukaji wa benki nchini. Wasimamizi wazuri wa mabenki ni wale wanaoruhusu benki zenye matatizo kuanguka haraka. Hata hivyo, Benki Kuu chini ya usimamizi wa Gavana inafanya kila linalowezekana kusimamia shughuli za benki nchini kwa ufanisi na kwa ujumla imefanya kazi nzuri sana katika usimamizi wa sekta hii nchini.

KUHUSU UNUNUZI WA NDEGE YA SERIKALI NA RADAR KATIKA BAJETI YA 2003/04

Mheshimiwa Spika, hoja ilitolewa kwa maandishi na Dr. Willbrod Slaa (Mb).

Mheshimiwa Spika, Ndege ya Serikali bado haijanunuliwa, kwa kuwa taratibu za ununuzi hazijakamilishwa. Kwa hivyo, fedha zilizotengwa mwaka wa fedha wa 2002/03, Tshs. 7 bilioni, hazijatumika. Kwa mwaka wa fedha wa 2003/04 kiasi cha Shs. 2 bilioni zimetengwa kupitia Fungu la Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Gharama halisi ya RADAR ni dola za Kimarekani 39,451,000. Kati ya hizo tumekwishalipa dola 10 milioni na bakaa ya dola 29, 451,000 itaanza kulipwa mwaka wa fedha wa 2004/05. Mwaka ujao wa fedha 2003/04 tutaanza kulipa riba ya mkopo huo na bajeti yake ipo kwenye fungu 22 chini ya kifungu kidogo cha ‘commercial interest’.

SEKTA YA MADINI

Mheshimiwa Spika, eneo la madini limeongelewa na Waheshimiwa Wabunge wengi. Kwa ujumla Waheshimiwa Wabunge wameelezea wasiwasi uliopo kuwa, kiasi ambacho Serikali inapata kutokana na shughuli za kuchimba madini nchini ni kidogo sana, na kwamba inafaa Serikali ikapitia upya vivutio vilivyotolewa kwa wawekezaji katika sekta hiyo kwa lengo la kuhakikisha kwamba nchi yetu inafaidika na rasilimali hiyo.

Mheshimiwa Spika, kazi ya kuwianisha maslahi ya Taifa na ya wawekezaji katika sekta ya madini ni muhimu sana, hasa kwa sababu madini ni rasilimali inayokwisha. Kwa hiyo, serikali imeyapokea kwa dhati mawazo ya Waheshimiwa Wabunge na itawafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika labda nikumbushe kwamba, marekebisho kadha yamekwishafanywa katika mfumo wa kodi zinazotozwa katika sekta hii ya madini. Marekebisho yaliyofanywa katika miaka miwili iliyopita ni pamoja na yafuatayo:-

i) Serikali ilifuta utaratibu wa kurejesha mrahaba kwa kampuni ya madini inapokuwa na hali mbaya ya fedha (negative cashflow),

ii) Serikali imefuta utaratibu wa kuruhusu gharama zote za mtaji katika mwaka mmoja (100% capital expensing) wakati wa kukokotoa mapato kwa ajili ya kutoza kodi,

iii) Serikali imefuta unafuu wa ziada wa asilimia 15 ya gharama iliyosalia,

iv) Hivi sasa, makampuni ya madini hulipia kwanza kodi zote kwenye mafuta ya diesel na kurejeshewa baada ya kuthibitisha matumizi halisi kwa TRA.

Pamoja na hatua hizi, Serikali itaendelea kuifanyia tafakari hali ya uzalishaji katika sekta ya madini kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali inaangalia uwezekano wa kuwa na mitambo ya kupima ubora wa dhahabu hapa nchini (assaying facilities), na inaandaa utaratibu wa kukagua mchanga unaopelekwa nje wenye dhahabu, na ukaguzi kwa ujumla kuhusu shughuli na mienendo ya uwekezaji katika sekta hii. Maelezo zaidi yatatolewa na Waziri mwenye dhamana ya sekta hiyo.

NISHATI

Mheshimiwa Spika, eneo la nishati nalo limezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge wengi. Suala la umeme ni kubwa, muhimu na gumu. Ninachoweza kusema kwa leo ni kwamba Serikali inaliangalia suala hili kwa uzito mkubwa.

KODI YA MAENDELEO

Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi wa kufuta kodi ya maendeleo ni dhahiri kwamba kutakuwa na pengo katika mapato ya halmashauri nyingi hasa zile za miji na jiji. Serikali inaandaa utaratibu muafaka wa kufidia sehemu ya mapato hayo. Hata hivyo, napenda kuchukua fursa hii kuzitaka halmashauri zote kuongeza jitihada katika kukusanya mapato kutokana na vyanzo vya mapato walivyo navyo bila kubughudhi wananchi. Utafiti uliofanywa na kuthibitishwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, unaonyesha kwamba makusanyo ya kodi ya maendeleo yalikuwa chini ya malengo kwa kuwa hawakuwa tayari kulipa kodi hii. Aidha, imebainika kuwa baadhi ya vyanzo vya mapato kama vile ‘property tax’ haikusanywi kabisa au kiasi kinachokusanywa ni kidogo sana. Pamoja na uamuzi huu, ni muhimu wananchi wakaelewa kuwa bado wanajukumu la kuchangia maendeleo yao katika maeneo yao.

MAREKEBISHO

Mheshimiwa Spika, Serikali imesikiliza kwa makini na kutafakari hoja za Waheshimiwa Wabunge ambazo zimegusia maeneo mengi sana. Serikali imejitahidi kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. Pamoja na maelezo hayo, kwa kuzingatia uzito wa hoja zilizotolewa katika baadhi ya maeneo, Serikali imeamua kufanya marekebisho yafuatayo:-

1. Ushuru wa Forodha kwa Dawa ya Mbu ya Kuchoma kutoka nje:

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipendekeza kuongeza ushuru wa forodha kwa dawa za mbu za kuchoma zinazoagizwa kutoka nje kutoka asilimia 10 ya sasa hadi asilimia 15, kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani ambavyo vinatumia pareto ya Tanzania kutengeneza dawa za mbu za kuchoma.

Hata hivyo kwa kuzingatia mapendekezo ya Waheshimiwa Wabunge, ushuru huo sasa utabakia katika kiwango cha sasa cha asilimia 10.

2. Nyenzo za Kutengeneza Vyandarua:

Mheshimiwa Spika, imebainika kwamba nyenzo muhimu zinazotumika kutengeneza vyandarua ni NYUZI ambazo zinatumiwa pia na viwanda vingine vya nguo. Sio rahisi kutofautisha nyuzi zinazotumiwa na viwanda vya kutengeneza vyandarua na zile zinazotumiwa kutengeneza bidhaa nyingine za nguo.

Ili kusaidia viwanda vinavyotengeneza vyandarua humu nchini, viwanda hivyo vitatakiwa kuwasilisha HAZINA mahitaji yao na mchanganuo wa nyenzo za msingi wanazohitaji kama malighafi ili zipewe unafuu wa kodi kwa kutumia Tangazo la Serikali (Government Notice). Aidha, nieleze kwamba Dawa ya Ngao ya kuweka kwenye vyandarua haitozwi kodi yoyote.

3. Kodi kwenye Madawa ya Binadamu:

Mheshimiwa Spika, hivi sasa madawa ya TB, Malaria, Ukimwi pamoja na Kondom, hayana kodi yoyote. Dawa nyingine zote zinazotoka nje zinalipa ushuru wa forodha wa asilimia 10, na zimesamehewa VAT. Ushuru huu wa asilimia 10 umewekwa ili angalau kusaidia viwanda vya ndani visife kutokana na ushindani kutoka dawa za nje.

Hata hivyo, kwa kuzingatia umuhimu wa kupatikana kwa dawa za kuokoa maisha ya watu kwa wingi, na kwa bei nafuu, orodha ya dawa zitakazosamehewa kodi itaongezwa ili kusiwe tena na visingizio vya ukosefu wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za Serikali.

4. Ushuru wa Bidhaa (excise tax) kwenye matumizi ya simu za mkononi:

Mheshimiwa Spika, Serikali ilikuwa imependekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye matumizi ya simu za mkononi kutoka asilimia 5 ya sasa hadi asilimia 7. Kwa kuzingatia hoja za Waheshimiwa Wabunge, na vilio vya kampuni za simu na wateja wao, Serikali imeamua kuondoa ongezeko la kodi hiyo. Kwa hiyo, ushuru kwenye matumizi ya simu za mkononi unabaki asilimia tano kama ilivyokuwa tangu Julai 2002.

5. Ushuru wa Ngozi Ghafi (hides and skins):

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipendekeza kuanzisha mfuko wa kuendeleza mifugo na kuanzisha ushuru wa asilimia 15 kwenye ngozi ghafi (hides and skins) zinazosafirishwa nje ya nchi, na mapato yatokanayo na ushuru yataingizwa kwenye mfuko huo (Livestock Development Fund). Ili mfuko huo uweze kuwa na manufaa katika kipindi cha muda mfupi, Serikali imeona ni vyema kuongeza ushuru huo hadi asilimia 20.

6. Udhibiti wa Ukwepaji wa Kodi ya Mafuta ya Petroli:

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipendekeza Bungeni hatua kadhaa kabambe za kudhibiti wimbi la ukwepaji wa kodi katika biashara ya mafuta ya petroli. Moja ya hatua hizo ni kwamba mafuta yote ya petroli yatakayoingizwa nchini yatakadiriwa kodi zote zinazostahili pale yanapoingia, na wenye mafuta watapewa Ankara (invoice) za kulipia kodi hiyo ambayo watapaswa walipe katika muda usiozidi siku kumi na tano (15). Baada ya kutafakari hoja za Waheshimiwa Wabunge na kampuni za mafuta, Serikali imeona ni bora muda huo wa kulipa kodi (grace period) uongezwe kutoka siku 15 hadi siku 30.

7. Msamaha wa VAT kwa “Sub-Contractors” wa Uchimbaji wa Madini:

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipendekeza kuingiza “sub-contractors” wanaoajiriwa na makampuni ya madini kwenye msamaha wa VAT. Kwa kuzingatia hoja za Waheshimiwa Wabunge kuhusu sekta ya madini, hatua hiyo sasa inasitishwa. “Sub-contractors” wataendelea kulipa VAT kama kawaida.

8. MWISHO:

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

0 comments:

Post a Comment