Tuesday, October 5, 2010

Kongamano la wanavyuo kumuunga mkono Mnyika


Mgombea Ubunge kwa jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA,John Mnyika akizungumza kwenye kongamano hilo la wanafunzi lililofanyika mwishoni mwa wiki lililoongelea maswala mbalimbali kuhusu Uchaguzi Mkuu 2010.
Dkt.Kitila Mkumbo, naye alishiriki na kuichambua kwa kina sera za chama cha CHADEMA. Miongoni mwa mengi ya msingi aliwaasa vijana kuwa wao ni chachu ya mabadiliko, lazima washiriki bega kwa bega kuhakikisha kuwa wanachagua mbunge atakaye kuwa mstari wa mbele kwa sauti yao-kuhakikisha anatetea maslahi ya wanavyuo na vijana wa Tanzania kwa ujumla.

Wanafunzi wa vyuo mbalimbali walifanya Kongamano la Wanafunzi jmwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rungwe kuongelea maswala mbalimbali kuhusu Uchaguzi Mkuu 2010. Vijana wapatao 200 walihudhuria na kutoa tamko la kumuunga mkono Mnyika katika harakati zake za kampeni jimbo la Ubungo.

0 comments:

Post a Comment