Thursday, October 28, 2010

FFU WATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIMSUBIRI DK SLAA IRINGA MJINI

Na Francis godwin, mzee wa matukio

FFU WATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIMSUBIRI DK SLAA IRINGA MJINIFFU wakipita mitaani eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimsubiri DK SLAA leo
Hapa wananchi wakitawanyika baada ya FFU kuwataka kutawanyika katika uwanja huo
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kufika Dk Slaa leo


ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) leo wamelazimika kuwatawanya maelfu ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambao walikuwa wakiendelea kumsubiri mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) Dk Willibrod Slaa katika uwanja wa Mwembetogwa.

Huku wananchi wa eneo la Kihesa wakilazimika kumzua mgombea huyo wa nafasi ya Urais Dk Slaa wakimlazimisha kuhutubia majira ya saa 1.20 usiku wakati akitokea uwanja wa Ndege Nduli.

Wananchi hao ambao walifika katika uwanja huo wa mikutano yapata majira ya saa 6 mchana waliendelea kumsubiri mgombea huyo wa nafasi ya Urais huku wakiimba nyimbo za kumkaribisha Ikulu jambo lililopelekea askari wa FFU ambao walikuwepo kwa wingi katika mkutano huo kwa ajili ya kuulinda mkutano huo kulazimika kutumia vipaza sauti kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kusubiri hadi majira ya saa 1 usiku wakiamini kuwa mgombea huyo angefika kuwahutubia.

Kabla ya wananchi hao kutawanywa na FFU mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao walipata kuwaomba radhi wananchi hao kuwa mgombea huyo ambaye alikuwa akitokea Dodoma amechelewa kufika kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wake .

Askari hao wakiwa katika magari zaidi ya matatu huku wakiwa wameshehena mabomu ya machuzi katika nguo zao waliwataka wananchi hao kuondoka katika eneo hilo kabla ya kutumia nguvu zaidi katika kuwatawanya huku baadhi ya magari yakizunguka katika mitaa mbali mbali wakipiga king’ora kuashiria hali ya hatari .

Hata hivyo kwa mujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao mgombea urais huyo wa Chadema atafanya mkutano wake huo wa kampeni kesho majira ya asubuhi katika viwanja hivyo na kuwaomba radhi wananchi ambao walijitokeza kwa wingi katika uwanja huo .

Alisema kuwa baaada ya kumaliza mkutano huo ambao kimsingi ulipawa kufanyika leo ataendelea katika jimbo la Njombe Magharibi linalogombewa na Thomas Nyimbo (Chadema) na kufanya mikutano katika kata karibu zote za jimbo hilo kama sehemu ya kuhitimisha kampeni zake ndani ya mkoa wa Iringa.

Awali mgombea ubunge katika jimbo hilo la Iringa mjini akiwahutubiwa wananchi hao awalitaka kutoichagua CCM katika jimbo hilo jumapili na kuwa pamoja na mbinu chafu za CCM kugawa fulana na vyakula ila bado amewataka wananchi kukihukumu chama hicho jumapili.

DK Slaa kabla ya kuingia mkoani Iringa jana alikuwa na mikutano yake ya mwisho ya kusisitiza watazania kujitokeza kwa wingi jumapili kuchagua Chadema ambapo alianza katika mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Temeke, Morogoro ,Dodoma na mkutano wa mwisho ulipaswa kufanyika mkoa wa Iringa katika viwanja hivyo vya Mwembetogwa .

0 comments:

Post a Comment