Thursday, October 28, 2010

Dr slaa; live dodoma leo saa 10.00 alasiri!

dk slaa anasubiriwa na umati wa watu hapa mjini dodoma kwenye viwanja vya barafu, vinavyopakana na uwanja wa jamhuri; uwanja uliokuwa mali ya mlipa kodi wa nchi hii ukapokwa.

inesemwa ya kwamba dk ws atawasili hapa majira ya saa 10:00 alasiri akitokea iringa.


nusu saa iliyopita nilikuwa hapo uwanjani nikashuhudia haya:

* umati wa watu ni mkubwa sana na hasa vijana.
* kuna malalamiko kuhusu kununuliwa kwa bendera za chadema kwa gharama kati ya sh.2000 hadi 10000 na watu ambao mshereheshaji anawaita mafisadi (unawajua!!!).
* wagombea udiwani wa kata mbali mbali wamepata nafasi ya kuwasalimia wananchi na kuomba kura kwa chadema.
* msisitizo umeelekezwa kwenye AMANI; ambapo wananchi wameombwa na wagombea, viongozi wa chadema na mshereheshaji kutokuwa chanzo cha machafuko.
* eneo la upande wa magharibi (uwanja wa jamhuri) na kusini kuna bendera za ccm.
* magari ya mashabiki wa ccm yanapita mara kwa mara yakifungulia sauti ya juu wimbo wao ule maarufu wa wa kuwachanachana watanzania wazalendo wanaoamua kujiunga na vyama vya upinzani kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
* kuna umati wa wapanda baiskeli na wale wa pikipiki zenye bendera ya chadema.


nawasilisha!!!

0 comments:

Post a Comment