Zifuatazo ni mbinu zitakazotumika kuiba kura kesho na zimeanza kutumika mkoani Shinyanga!!!
1.0  Mabalozi wote wa nyumba 10 na viongozi wa serekali za mitaa wanaitwa,  wanapewa karatasi 2 za kupigia kura zilizo na vema tayari kwa mgombea wa  kijani. Karatasi moja ni ya mume na moja ni ya mke wake. Kesho kila  mmoja atakapoingia chumba cha kupiga kura atatakiwa achukue karatasi  ingine (ya awali atakuwa kaificha). Akisha piga kura, atadumbukiza  kwenye sanduku karatasi zote mbili. Hivyo mjumbe mmoja atapiga kura 2 na  mkewe/mumewe kura 2. Jumla 4
Chadema wafanyeje kudhibiti  hali hii??? Waweke daftari ambalo kila anaeingia anaandika namba kuanzia  1 hadi mtu wa mwisho. Baada ya kuhesabu kura, zitakazozidi zitakuwa ni  zile zilizochakachuliwa!!!!!
Kama itawezekana, kila mpiga  kura akaguliwe idadi ya karatasi atakazotumbukiza kwenye sanduku la  kupigia kura. Else, wawakague watu kabla hawajawapa karatasi za kupigia  kura, kujiridhisha kwamba, hawana vibomu/videsa vya ziada.
Its  serious vikao vinaendelea kutimiza azma ya kupiga kura kwa design hiyo,  japo maeneo yaliyolengwa ni yale yenye upinzani wa kweli. Mf.  Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mwanza na Mara.  DSM inaogopwa sababu ya  mwamko na kusambaa kwa taarifa sababu ya teknologia!!
2.  Mbinu ya pili ni kutoa karatasi za kupigia kura zisizo na muhuri  sambamba na zenye muhuri wa tume ya uchaguzi, ambapo karatasi zisizokuwa  na muhuri zitachukuliwa kuwa batili kwa sababu hazijapigwa muhuri wa  NEC.
Chadema wafanye nini hapa!!! Kila mtu anapofika kupiga  kura, mawakala wapitie kila karatasi anayopewa mpiga kura kuhakikisha  kwamba karatasi anayopewa mpiga kura ina muhuri sahihi.
3.  Kuchakachua kura zikiwa njiani kwenda kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa  jimbo!!! Kwenye sheria za NEC na taratibu za internal control (Sarbanese  Oxley Act), hapa kuna leakage. Hakuna anaeweza kuthibitisha kuto  kuchakachuliwa kwa masanduku ya kura njiani kwakuwa mawakala hawana  uwezo kusindikiza kura hizo!!!
Naomba kuwashirikisha mbinu hizo chafu kutokea Shinyanga!!! Hali si hali
Mungu awalinde na kuwabariki, awawezeshe nyote kupiga kura kwa umakini na kwa amani na kumpata Raisi wa kutuongoza kwa kipindi kijacho cha miaka mi tano mwenye hekima, akili, busara na hofu ya Mungu ndani yake!!!
0 comments:
Post a Comment