Thursday, October 21, 2010

MGOMBEA UBUNGE NCCR Mageuzi aunganisha nguvu CHADEMA - Sumbawanga MjiniWAKATI wagombea watatu wa CCM ,CUF na UDP wakikwepa kufika katika mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa mgombea wa NCCR-Mageuzi Kiyaya Dominic (kulia) amewataka wananchi wa jimbo hilo kura zake zote kumpa mgombea wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) Mwalimu Norbart Yamsebo (kushoto mwenye shati jekundu)

Pamoja na kuwaomba wananchi kumchagua mgombea wa Chadema kwa kuwa ndiye mwenye sifa za kuliongoza jimbo hilo pia amemwomba radhi mwenyekiti wa Taifa wa NCCR –Mageuzi James Mbatia kutoka na uamuzi wake wa kumuunga mkono mgombea mwenzake wa Chadema katika jimbo hilo.

Dominic ambaye pia ni katibu wa NCCR-Mkoa wa Rukwa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Sumbawanga mjini ,mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Rukwa (RANGO) kwa ufadhili wa jumuiko la asasi za Kiraia Tanzania uliofanyika ukumbi wa Bethelehem Centre mjini Sumbawanga.

Alisema kuwa pamoja na chama chake kumwamini na kumsimamisha kugombea jimbo hilo ila bado amejipima na kuona kuwa hana uwezo kushindana na mgombea wa chama kisifa na kupendwa na wannachi na kuwaomba hata wagombea wenzake akiwemo wa CCM Aesh Hillary kumuunga mkono mgombea huyo wa Chadema.

“Mwenyekiti wangu Mbatia na wananchi pamoja na wanachama wa NCCR-Mageuzi …..naomba sana msinichukulia tofauti siasa sio vita na lazima mwanasiasa mzuri usome alama za nyakati pia ….hapa Sumbawanga mjini mwenye sifa ya kuwa mgombea mwalimu Yamsebo ….hivyo lazima sisi wengine kumuunge mkono”

Hata hivyo alisema kuwa muda wa kampeni uliobaki ataendelea kufanya kampeni kama kawaida ila zitakuwa ni kameni za kumnadi mgombea huyo wa Chadema na kumwombea kura kwa wananchi.

Kwa upande wake Yamsebo mbali ya kumpongeza mgombea huyu wa NCCR –Mageuzi kwa kukubali yaishi bado alimwomba mgombea wa CCM kuiga mfano huo badala ya kusubiri kushindwa kwa aibu.

Source:Francis Godwin ni mzee wa matukio daima

0 comments:

Post a Comment