Saturday, October 16, 2010

MGOMBEA URAISI WA CHADEMA DR W P SLAA ALIPOFIKA TABORA LEO

Dr Slaa ameingia Tabora mjini saa 11:50 jioni,
amepokelewa kwa bashasha kubwa na wananchi wa Tabora...
Mshehereshaji ajapoteza muda, na kumkaribisha Dr Slaa Jukwaani..
Dr anaanza kwa kuomba samahani kwa kuchelewa kufika akitokea Urambo, na wananchi kuridhia kumsamehe...
Huku akiwa anaonekana anaharaka sana, anaanza kwa kumwaga sera moja kwa moja..
Ameanza kwa kutoa ahadi ya kupunguza kodi ya vifaa vya ujenzi, na kufafanua kwa kina.. Ila muda ndo hautoshi..
Huku akionekana ni mwenye afya tele..
Anaelezea pia anaufahamu sana mji wa Tabora, amesomea hapa, seminari ya Itaga, na Kipalapala, anashangaa kuona mji aliouacha umezidi kudidimia kiuchumi, na kimaendeleo...
Anaendelea na sera ya ahadi ya kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto anaeenda shule..
Anaendelea kuvuta hisia za watu wa hali ya chini, kwa kutoa pia ahadi ya kutetea wanyonge na mali zao...
Muda unazidi kwenda kasi, huku giza likianza ingia, wananchi nao wanaendelea kua wavumilivu kumsikiliza...
Anamwita Mgombea ubunge jimbo la Tabora Mjini, na kumtambulisha ndugu Gwikima, na watu kumhaidi kua watampa kura zao...
Baada ya hapo anamwita mke wake Bi josephine na kumtambulisha mbele ya wananchi na kumpa kipaza sauti ajitambulishe mwenyewe.. Wananchi...
Huku akionekana mwenye haraka, anamponda mgombea wa CCM, kwa kukiuka muda, na kuwaomba wananchi waendelee kumsikiliza hata mpaka saa 5 usiku, huku akionekana jasiri, anasema yupo tayari kujibu kwa tume..
Anamaliza kwa kuwapa wananchi somo la uraia na wasifanye makosa octoba 31..
Huwezi amini, wananchi wanasukuma gari la Dr Slaa , gari likiwa limezimwa, hakika wananchi ni Wengi sana..
Mkutano unaisha muda huu..

GONGA HAPA KWA HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment