Friday, October 29, 2010

FFU WAKIMBIZA WAFUASI WA CHADEMA IRINGA ,DK SLAA AKWAMA KUHUTUBIA

"
Hapa tupo gado akitua tu Dk Slaa tunaye"
"
Ila hawa wananchi mbona ni wengi sana itakuwaje hawawezi kufanya fujo"
"
Jamaa hakuna kulala hadi kieleweke twendeni uwanja mwingine kama huu hapa wamezuia"
"
Mzee salama hapa ama ?kwani kuna nini ni vita ?"
"
Hapa tupo kamili kwa lolote "kama wanazungumza

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Iringa wakiwa wamejipanga kwa lolote katika viwanja vya uwanja wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa ambako ulipangwa mkutano wa mwisho wa mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa ambaye hata hivyo hakuweza kutua katika uwanja huo kama njia ya kukepa mbinu za CCM kutaka kuvuruga mkutano wake huo iwapo angetua katika uwanja huo leo asubuhi
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba vyao vya madarasa kuhofu usalama wao baada ya polisi wa FFU kutanda kuzunguka majengo ya shule hiyo ambayo yapo jirani na uwanja wa mkutano uliokuwa ukifanywa na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya mgombea urais Dk Willibrod Slaa kushindwa kutua kuhofu fujo kati yake ya polisi hao ambao walikuwa wakipinga mkutano huo kuhutubiwa na mgombea urais
Polisi wa FFU wakilinda eneo la mkutano ambao lilipaswa kuhutubiwa na mgombea urais wa Chadema Dk Slaa ambaye hata hivyo ameshindwa kuhutubia katika viwanja hivyo vya Mlandege
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege wakichungulia madirishani baada ya walimu wao kukimbia madarasani kuhofu mabomu muda mfupi baada ya FFU kutua eneo hilo na kuwataka wananchi kutawanyika kabla ya viongozi wa Chadema kujitoa mhanga na kuangua kilio cha kuomba msahama mbele ya askari hao
Hapa uwanja wa Mwembetogwa Iringa ambako ilipaswa Dk Slaa kufanya mkutano wake wa kampeni leo asubuhi japo imeshindikana
Askari wa FFU mjini Iringa wakiwa wamepiga kambi katika uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mgombea urais wa Chadema Dk Slaa kufanya mkutano eneo hilo ,kulia ni mwananchi akijikaza kupita kiume eneo hilo ambalo wananchi walitawanywa .




Na Francis Godwin,Iringa


NGOMA nzito Iringa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa amegonga mwamba kutaka kufanya mkutano wa kampeni bila kibali katika viwanja viwili tofauti mjini Iringa, baada ya Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda katika viwanja vyote kuzuia mikutano hiyo kwa madai kwamba haina baraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.



Polisi waliokuwa na silaha kali na mabomu ya kutoa machozi, walifanikiwa kuwatawanya maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakiendelea kukusanyika kwa wingi katika uwanja wa Mwembtogwa mjini hapa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Baada ya kutawanywa, wananchi hao walielekea katika uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege walikotangaziwa kwamba Dk Slaa angetumia jukwaa la mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa, kuwasalimia wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kabla hajaendelea na ziara yake ya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Njombe Kaskazini, Njombe Magharibi na Songea Mjini.

0 comments:

Post a Comment