Saturday, October 9, 2010

VYOMBO VYA HABARI VYAONYWA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI

Na Tiganya Vincent-MAELEZO

Dar es salaam.


Serikali imeonya vyombo vya habari kuacha mara moja kuandika habari za uchochezi unaolenga kuwachonganisha wananchi na Serikali yao iliyopo madarakani.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bw.Sethi Kamuhanda wakati mkutano wake na wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania(TSN) kwenye ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni hiyo.

Alisema kuwa ni vema vyombo vya habari vikafanya kazi hapa nchini kutoa habari zinazozingatia weledi wa taalum ya uandishi wa habari na sio kupandikiza uchochezi miongoni mwa Watanzania na hivyo kuzorotesha amani.


Kamuhanda alisema kuwa Serikali haitavumilia hali ya uchochezi inayofanywa na baadhi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa wageni na vile vya ndani vinavyopandikiza chuki na kuichafua Tanzania.

"Tunaomba vyombo vya habari vyote ambavyo vimefanya uchochezi kuwa sehemu ya professional kuacha mara moja kwani wakitulazimisha tuvifungia au kufuta katika usajili ...tunawaomba kuandika habari ambazo hazina uchochezi na zinazozingatia taratibu na Sheria zilzopo" alisisitiza Katibu Mkuu huyo.Alisema kuwa pamoja na uhuru uliopo kwa vyombo vya habari nchini ni vema wakautumia vizuri badala ya kugeuza vyombo vya habari kuwa uwanja wa uchochezi unaotishia amani.


Kamuhanda alitoa mfano kuwa kuwa baadhi ya Nchi zijikuta katika machafuko na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya vyombo vya habari vilivyofanya uchochezi kuwa kama ajenda yao kubwa na kuongeza kuwa Serikali halifumbia macho chombo cha habari chenye mlengo huo.Hata hivyo alisema Serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na kusajili vingine vingi ili cha msingi kwa waandishi wa habari ni kuzingatia weledi wa uandishi wa habari ili uhuru huo ulete maana halisi.


Kwa upande wa wananchi walitoa maoni yao kuhusu agizo hilo la Katibu Mkuu walisema kuwa tamko hilo ni vema likaanza kutekelezwa kwani wamechochosa na baadhi ya vyombo vya habari kugeuzwa majukwaa ya kupandikiza chuki katik ya kundi moja na lingine.

0 comments:

Post a Comment