Wednesday, October 27, 2010

DR SLAA ALIVYOTIKISA MWEMBEYANGA

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni leo mchana.
Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo jioni.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke leo jioni.Picha kwa hisani ya Joseph Senga wa Tanzania Daima.

1 comments:

cyprian m.e said...

tena huko mwembe yanga kuna wapenzi kibao wa chadema ila wanataka mabadiliko makubwa kwa kuwa eneo hilo linaonekana kusahaulika katika ramani ya tanzania ,kwa mfano ukiangalia hizo barabara,maji na maeneo hayana mitaro na mvua ikinyesha inakuwa balaa hasa magonjwa ya mlipuko yakianza

Post a Comment