Saturday, October 2, 2010

DR SLAA AITEKA NJOMBE

Helkopta ya mgombea urais wa Chadema Dr.Slaa ikitua katika uwanja wa mkutano asubuhi hii
Wananchi wa Njombe wakiipungia mikono Helkopata ya Dr Slaa
Dr Slaa akipokelewa na viongozi wa wilaya ya Njombe mara baada ya kuwasili dakika chache kuanzia sasa
Helkopta ya Mgombea Urais wa Chadema ikiwa hewani ikijiandaa kutua uwanja wa Mdete Njombe mjini

Mgombea urais kwa Chadema Dr Willbroad Slaa amemshukia mkuu wa mnajimu mkuu wa majeshi nchini Bw Shimbo kuwa ndani ya siku 10 awe amewakamata wale wote ambao wanatuhumiwa kumwaga damu na vinginevyo hatua itachukuliwa dhidi yake.

Pia Dr.Slaa amesema kuwa CCM imepanga kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu na ndio sababu ya kuanza kutumia vyombo vya habari vya umma ,majeshi na usalama wa Taifa kuweka kinga na kuwa kama CCM imepanga kuchakachua matokeo basi itachakachuliwa yenyewe .

Hata hivyo ameonya jeshi la Poliso kupitia wakuu wa polisi wilaya kuwa kama wanapewa taarifa na kuchanwa mabango ya wagombea bila kuchukua hatua ni mwanzo wa jeshi la polisi kuchochea vurugu na kuwa Chadema kamwe haitafanya fujo labda fujo zitoke CCM.

Dr.Slaa ambaye anaendelea na hutuba yake viwanja wa Mdete mjini Njombe anaema kuwa hatautamani Urais wa Tanzania kama damu ya watanzania itamwagika katika uchaguzi na kuwa Chadema imejipanga kulinda amani na kuwa Green gadi ya CCM ni mwanzo wa fujo katika uchaguzi agiza polisi kuwakamata

video video video

0 comments:

Post a Comment