Sunday, October 31, 2010

HABARI/TAARIFA ZA UCHAGUZI TANZANIA 2010

Matokeo yaanza kutangazwa

Matokeo yaanza kutangazwa - ZANZIBAR/PEMBA

TUME YA UCHAGUZI IMEBORONGA

NAMBA ZA MAKAO MAKUU CHADEMA

01: Mbogo: 0683-179001, 0714-776673
02: Mahinda: 0715-949019
03: Dady Igogo: 0713-616096
04: John Mnyika: 0754-694553

Fuatilia mwenendo kwa kugonga


Taarifa / Habari za Uchaguzi Mkuu - Upigaji Kura

State of the Nation Report 31st October 2010

www.wanabidii.net


Saturday, October 30, 2010

Mbinu zinazoweza Kutumika Kuiba Kura

Zifuatazo ni mbinu zitakazotumika kuiba kura kesho na zimeanza kutumika mkoani Shinyanga!!!

1.0 Mabalozi wote wa nyumba 10 na viongozi wa serekali za mitaa wanaitwa, wanapewa karatasi 2 za kupigia kura zilizo na vema tayari kwa mgombea wa kijani. Karatasi moja ni ya mume na moja ni ya mke wake. Kesho kila mmoja atakapoingia chumba cha kupiga kura atatakiwa achukue karatasi ingine (ya awali atakuwa kaificha). Akisha piga kura, atadumbukiza kwenye sanduku karatasi zote mbili. Hivyo mjumbe mmoja atapiga kura 2 na mkewe/mumewe kura 2. Jumla 4

Chadema wafanyeje kudhibiti hali hii??? Waweke daftari ambalo kila anaeingia anaandika namba kuanzia 1 hadi mtu wa mwisho. Baada ya kuhesabu kura, zitakazozidi zitakuwa ni zile zilizochakachuliwa!!!!!

Kama itawezekana, kila mpiga kura akaguliwe idadi ya karatasi atakazotumbukiza kwenye sanduku la kupigia kura. Else, wawakague watu kabla hawajawapa karatasi za kupigia kura, kujiridhisha kwamba, hawana vibomu/videsa vya ziada.

Its serious vikao vinaendelea kutimiza azma ya kupiga kura kwa design hiyo, japo maeneo yaliyolengwa ni yale yenye upinzani wa kweli. Mf. Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mwanza na Mara. DSM inaogopwa sababu ya mwamko na kusambaa kwa taarifa sababu ya teknologia!!

2. Mbinu ya pili ni kutoa karatasi za kupigia kura zisizo na muhuri sambamba na zenye muhuri wa tume ya uchaguzi, ambapo karatasi zisizokuwa na muhuri zitachukuliwa kuwa batili kwa sababu hazijapigwa muhuri wa NEC.

Chadema wafanye nini hapa!!! Kila mtu anapofika kupiga kura, mawakala wapitie kila karatasi anayopewa mpiga kura kuhakikisha kwamba karatasi anayopewa mpiga kura ina muhuri sahihi.

3. Kuchakachua kura zikiwa njiani kwenda kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo!!! Kwenye sheria za NEC na taratibu za internal control (Sarbanese Oxley Act), hapa kuna leakage. Hakuna anaeweza kuthibitisha kuto kuchakachuliwa kwa masanduku ya kura njiani kwakuwa mawakala hawana uwezo kusindikiza kura hizo!!!

Naomba kuwashirikisha mbinu hizo chafu kutokea Shinyanga!!! Hali si hali

Mungu awalinde na kuwabariki, awawezeshe nyote kupiga kura kwa umakini na kwa amani na kumpata Raisi wa kutuongoza kwa kipindi kijacho cha miaka mi tano mwenye hekima, akili, busara na hofu ya Mungu ndani yake!!!

Kampeni ya Mwisho ya DR W P SLAA Mkoani Mbeya








Amri kumi za Uchaguzi

1. Tambua kwamba kura ni silaha takatifu inayokuwezesha kumchagua yule
unayeamini kwamba unaweza kumkabidhi sehemu ya maisha yako na ukawa salama.
Tumia busara.

2. Jua kwamba ni usaliti kwako mwenyewe na kwa wananchi wengine iwapo
utapiga kura kwa misingi ya rushwa. Anayekununua hakuthamini. Kwake wewe ni
bidhaa tu, kama maharage.

3. Usiruhusu hisia za ubaguzi wa kabila, rangi, dini, jinsia, au ubaguzi wa
aina yoyote nyingine ili utawale uamuzi wako katika kupiga kura.

4. Tenda haki kwa wengine, na pia dai haki yako kutoka kwa wengine.
Usimwonee yeyote na wala usimruhusu yeyote akuonee.

5. Watetee na walinde wanyonge na wasiojiweza. Wasaidie ili waweze kutumia
haki yao ya kupiga kura.

6. Imarisha uhuru wako na uhuru wa nchi yako kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi
unakuwa na maana, na kwamba kila kura inayopigwa ina maana.

7. Epuka vurugu, vitisho na ugomvi. Kura ni jambo la raha, si karaha.

8. Kumbuka kwamba amani ni mwana wa haki. Penye haki, aliyeshindwa akubali
kushindwa, na aliyeshinda bado atende haki kwa aliyeshindwa.

9. Tambua kwamba uchaguzi unakuja na kwisha, viongozi huja na kuondoka,
lakini Taifa na watu wake hudumu milele. Tuliza hamasa, epuka chuki, uwe na
ustahimilivu.

10. Hii ni fursa adhimu; ifurahie.

JENERALI ULIMWENGU

Kipindi maalumu kwenye ITV na Dk Slaa (Saa 9.30 hadi Saa 10.30)

Kutakuwa na kipindi maalumu cha Dk Slaa katika ITV leo siku ya mwisho wa kampeni kuanzia saa 9.30 hadi saa 10.30 jioni. Katika kipindi hiki Dk Slaa atafanya majumuisho ya kampeni zake na kuwaomba tena watanzania wamchague hiyo kesho.

Awali kipindi hiki kilikuwa kirushwe kuanzia saa 11 hadi saa 12, lakini katika hali ya kushangaza, ghafla ITV wameomba radhi kwamba kipindi hiki hakiwezi kuonyeshwa katika muda uliokubaliwa awali. Habari zilizopo ni kwamba CCM wakiongozwa na Kinana wameenda leo asubuhi kuwaomba ITV wasionyeshe hicho kipindi katika muda huo na wakaomba ITV waungane na TBC kurusha mkutano wa JK live Jangwani. Safari ya ukombozi ni ndefu lakini lazima tuitembee.

Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimena mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

Friday, October 29, 2010

MIJADALA MBALIMBALI

GONGA LINKI KWA HABARI ZAIDI

MBINU ZA VITUO HEWA VYA KUPIGA KURA WAGUNDULIKA KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

WANANCHI WENZANGU, SAFARI HII TUSIDANGANYIKE!

Kura zimeshaibwa, Kikwete 80% ameshinda!

Mbinu chafu za CCM jimbo la Ubungo

FFU WAKIMBIZA WAFUASI WA CHADEMA IRINGA ,DK SLAA AKWAMA KUHUTUBIA

"
Hapa tupo gado akitua tu Dk Slaa tunaye"
"
Ila hawa wananchi mbona ni wengi sana itakuwaje hawawezi kufanya fujo"
"
Jamaa hakuna kulala hadi kieleweke twendeni uwanja mwingine kama huu hapa wamezuia"
"
Mzee salama hapa ama ?kwani kuna nini ni vita ?"
"
Hapa tupo kamili kwa lolote "kama wanazungumza

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Iringa wakiwa wamejipanga kwa lolote katika viwanja vya uwanja wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa ambako ulipangwa mkutano wa mwisho wa mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa ambaye hata hivyo hakuweza kutua katika uwanja huo kama njia ya kukepa mbinu za CCM kutaka kuvuruga mkutano wake huo iwapo angetua katika uwanja huo leo asubuhi
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba vyao vya madarasa kuhofu usalama wao baada ya polisi wa FFU kutanda kuzunguka majengo ya shule hiyo ambayo yapo jirani na uwanja wa mkutano uliokuwa ukifanywa na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya mgombea urais Dk Willibrod Slaa kushindwa kutua kuhofu fujo kati yake ya polisi hao ambao walikuwa wakipinga mkutano huo kuhutubiwa na mgombea urais
Polisi wa FFU wakilinda eneo la mkutano ambao lilipaswa kuhutubiwa na mgombea urais wa Chadema Dk Slaa ambaye hata hivyo ameshindwa kuhutubia katika viwanja hivyo vya Mlandege
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege wakichungulia madirishani baada ya walimu wao kukimbia madarasani kuhofu mabomu muda mfupi baada ya FFU kutua eneo hilo na kuwataka wananchi kutawanyika kabla ya viongozi wa Chadema kujitoa mhanga na kuangua kilio cha kuomba msahama mbele ya askari hao
Hapa uwanja wa Mwembetogwa Iringa ambako ilipaswa Dk Slaa kufanya mkutano wake wa kampeni leo asubuhi japo imeshindikana
Askari wa FFU mjini Iringa wakiwa wamepiga kambi katika uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mgombea urais wa Chadema Dk Slaa kufanya mkutano eneo hilo ,kulia ni mwananchi akijikaza kupita kiume eneo hilo ambalo wananchi walitawanywa .




Na Francis Godwin,Iringa


NGOMA nzito Iringa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa amegonga mwamba kutaka kufanya mkutano wa kampeni bila kibali katika viwanja viwili tofauti mjini Iringa, baada ya Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda katika viwanja vyote kuzuia mikutano hiyo kwa madai kwamba haina baraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.



Polisi waliokuwa na silaha kali na mabomu ya kutoa machozi, walifanikiwa kuwatawanya maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakiendelea kukusanyika kwa wingi katika uwanja wa Mwembtogwa mjini hapa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Baada ya kutawanywa, wananchi hao walielekea katika uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege walikotangaziwa kwamba Dk Slaa angetumia jukwaa la mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa, kuwasalimia wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kabla hajaendelea na ziara yake ya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Njombe Kaskazini, Njombe Magharibi na Songea Mjini.

Thursday, October 28, 2010

Namuunga Mkono DR Slaa Asema Prof Lipumba wa CUF

Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF amesema anamuunga mkono
yule wa CHADEMA DR W P SLAA , Kwahiyo amewasihi wananchi wampigie kura dr
slaa kama wasipompa yeye ila kasema yeye ni kama Mlima wakati DR SLAA ni
Kichuguu ameyasema hayo katika Mdahalo maalumu unaorushwa na ITV Moja kwa
moja sasa hivi

Gonga hapa kufuatilia Mjadala Huu
Namuunga Mkono DR Slaa Asema Prof Lipumba wa CUF

Kituo Bandia cha Kupiga Kura Chagundulika Shinyanga

Kuna jamaa yangu ameniambia kwamba kuna taarifa za kugundulika kituo Bandia
( Feki ) Cha kupiga kura , Anasema wananchi wa maeneo hayo walikuta majina
yao yameandikwa mara 2 moja kwenye eneo lao na kopy ya pili kwenye eneo
lingine na kubandikwa ambako hakuna kutuo lakini majina yao yalibandikwa
hapo .

Hizi ni tetesi tu sijadhibitisha lakini watu wawe makini kwa kuangalia
vizuri vituo na majina yao

GONGA HAPA KUFUATILIA
Kituo Bandia cha Kupiga Kura Chagundulika Shinyanga

DK SLAA KUHUTUBIA WANANCHI WA MKOA WA IRINGA KUPITIA REDIO COUNTRY FM LEO SAA 3 USIKU



Baada ya kushindwa kuwahutubia wananchi wa manispaa ya Iringa leo jioni ,mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Dk Willibrod Slaa leo saa 3 usiku huu atawahutubia moja kwa moja wananchi wa mkoa wa Iringa kupitia kituo cha Redio Country Fm (88.5 ) wananachi watapata nafasi ya kumsikiliza na kuuliza maswali yao kaa mkao wa kula

FFU WATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIMSUBIRI DK SLAA IRINGA MJINI

Na Francis godwin, mzee wa matukio

FFU WATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIMSUBIRI DK SLAA IRINGA MJINI



FFU wakipita mitaani eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimsubiri DK SLAA leo
Hapa wananchi wakitawanyika baada ya FFU kuwataka kutawanyika katika uwanja huo
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kufika Dk Slaa leo


ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) leo wamelazimika kuwatawanya maelfu ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambao walikuwa wakiendelea kumsubiri mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) Dk Willibrod Slaa katika uwanja wa Mwembetogwa.

Huku wananchi wa eneo la Kihesa wakilazimika kumzua mgombea huyo wa nafasi ya Urais Dk Slaa wakimlazimisha kuhutubia majira ya saa 1.20 usiku wakati akitokea uwanja wa Ndege Nduli.

Wananchi hao ambao walifika katika uwanja huo wa mikutano yapata majira ya saa 6 mchana waliendelea kumsubiri mgombea huyo wa nafasi ya Urais huku wakiimba nyimbo za kumkaribisha Ikulu jambo lililopelekea askari wa FFU ambao walikuwepo kwa wingi katika mkutano huo kwa ajili ya kuulinda mkutano huo kulazimika kutumia vipaza sauti kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kusubiri hadi majira ya saa 1 usiku wakiamini kuwa mgombea huyo angefika kuwahutubia.

Kabla ya wananchi hao kutawanywa na FFU mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao walipata kuwaomba radhi wananchi hao kuwa mgombea huyo ambaye alikuwa akitokea Dodoma amechelewa kufika kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wake .

Askari hao wakiwa katika magari zaidi ya matatu huku wakiwa wameshehena mabomu ya machuzi katika nguo zao waliwataka wananchi hao kuondoka katika eneo hilo kabla ya kutumia nguvu zaidi katika kuwatawanya huku baadhi ya magari yakizunguka katika mitaa mbali mbali wakipiga king’ora kuashiria hali ya hatari .

Hata hivyo kwa mujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao mgombea urais huyo wa Chadema atafanya mkutano wake huo wa kampeni kesho majira ya asubuhi katika viwanja hivyo na kuwaomba radhi wananchi ambao walijitokeza kwa wingi katika uwanja huo .

Alisema kuwa baaada ya kumaliza mkutano huo ambao kimsingi ulipawa kufanyika leo ataendelea katika jimbo la Njombe Magharibi linalogombewa na Thomas Nyimbo (Chadema) na kufanya mikutano katika kata karibu zote za jimbo hilo kama sehemu ya kuhitimisha kampeni zake ndani ya mkoa wa Iringa.

Awali mgombea ubunge katika jimbo hilo la Iringa mjini akiwahutubiwa wananchi hao awalitaka kutoichagua CCM katika jimbo hilo jumapili na kuwa pamoja na mbinu chafu za CCM kugawa fulana na vyakula ila bado amewataka wananchi kukihukumu chama hicho jumapili.

DK Slaa kabla ya kuingia mkoani Iringa jana alikuwa na mikutano yake ya mwisho ya kusisitiza watazania kujitokeza kwa wingi jumapili kuchagua Chadema ambapo alianza katika mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Temeke, Morogoro ,Dodoma na mkutano wa mwisho ulipaswa kufanyika mkoa wa Iringa katika viwanja hivyo vya Mwembetogwa .

Dr slaa; live dodoma leo saa 10.00 alasiri!

dk slaa anasubiriwa na umati wa watu hapa mjini dodoma kwenye viwanja vya barafu, vinavyopakana na uwanja wa jamhuri; uwanja uliokuwa mali ya mlipa kodi wa nchi hii ukapokwa.

inesemwa ya kwamba dk ws atawasili hapa majira ya saa 10:00 alasiri akitokea iringa.


nusu saa iliyopita nilikuwa hapo uwanjani nikashuhudia haya:

* umati wa watu ni mkubwa sana na hasa vijana.
* kuna malalamiko kuhusu kununuliwa kwa bendera za chadema kwa gharama kati ya sh.2000 hadi 10000 na watu ambao mshereheshaji anawaita mafisadi (unawajua!!!).
* wagombea udiwani wa kata mbali mbali wamepata nafasi ya kuwasalimia wananchi na kuomba kura kwa chadema.
* msisitizo umeelekezwa kwenye AMANI; ambapo wananchi wameombwa na wagombea, viongozi wa chadema na mshereheshaji kutokuwa chanzo cha machafuko.
* eneo la upande wa magharibi (uwanja wa jamhuri) na kusini kuna bendera za ccm.
* magari ya mashabiki wa ccm yanapita mara kwa mara yakifungulia sauti ya juu wimbo wao ule maarufu wa wa kuwachanachana watanzania wazalendo wanaoamua kujiunga na vyama vya upinzani kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
* kuna umati wa wapanda baiskeli na wale wa pikipiki zenye bendera ya chadema.


nawasilisha!!!

Marando atinga Maswa kumsaidia Shibuda

Marando atinga Maswa kumsaidia Shibuda, baadae Mara na Mwanza atakapowakampenia familia ya Nyerere, Vicent (Musoma Mjini) na Leticia (Magu) na baadae kwenda kuhitimisha kwa Waziri Kijana Nyamagana ambako kunatarajiwa kutokea Waziri Kijana mbadala (Wenje)

KAMPENI MBALIMBALI ZA CHADEMA







WAGOMBEA WA CHADEMA 2010 NA MAJIMBO YAO

Namba JIMBO JINA LA MGOMBEA.
1. Moshi Mjini. Philemon Ndesamburo
2. Hai Freeman Mbowe
3. Moshi Vijijini. Anthony Komu
4. Rombo Joseph Selasini.
5. Vunjo John Mrema.
6. Mwanga Shafi Yaperi Msuya.
7. Siha Eng. Humprey Tuni.
8. Same Magharibi Eneza Elikunda Mshana.
9. Same Mashariki Naghenjwa Livingstone Kaboyoka.
10. Kiteto Victor Kimesera.
11. Mbulu Mustapha Akunaay
12. Hanang Rose Kamili
13. Babati Mjini Pauline Philipo Gekul
14. Babati Vijijini Francis Peter Qamara
15. Kigoma Kaskzn Zitto Kabwe
16. Kigoma Ujiji Ally Khalifani
17. Kigoma Kusini Muslim Hassanal
18. Muhambwe Arcardo Ntagazwa
19. Kasulu Mjini Ishimaili Jonathan Luyagaza.
20. Kasulu Vijijini Thadeo Gaudence Lukimisha.
21. Buyungu Revocatus Sylivanus Masunzu
22. Kasulu Magharibi Basilus Budidantizirusha Budida
23. Tarime Mwita Mwikwabe
24. Rorya Martine Ochola Ndira.
25. Musoma Mjini. Vincent Nyerere.
26. Mwibara David Chiriko
27. Bunda Elias Kajeri Maarungu
28. Serengeti Marwa Ryoba Chacha
29. Musoma Vijijini Michael M. Makenji
30. Ubungo John Mnyika.
31. Kawe Halima Mdee.
32. Ukonga James Binagi
33. Kinondoni Philip Nyanchini Mogendi
34. Kigamboni Maulidah Komu.
35. Ilala Naomi Kaihula.
36. Temeke Dikson Ng’hilly
37. Segerea Fred Mpendazoe.
38. Ukerewe Eng. Salvatory Machemuli.
39. Kwimba Leticia Nyerere
40. Nyamagana Ezekiah Wenje
41. Buchosa Martine Kaswahili
42. Geita Florence Msabila
43. Ilemela Hyness David Kiwia
44. Magu Ndimanya Bahati
45. Busega Jacta Katinde Levi.
46. Nyang’hwale Nduru Bright Tanganyika
47. Busanda Finias Magessa.
48. Sengerema.
49. Misungwi Jane Deogratias Kajoki.
50. Sumve Milton Fikiri Lutabana.
51. Muleba Kaskzn Msedemu Milanga
52. Karagwe Deusdedit Jovin
53. Bukoba Mjini Wilfred Lwakatare
54. Kyerwa Innocent kato
55. Nkenge Walter Nyahoza.
56. Bukoba vijijini Artides Ndibalema
57. Biharamulo Magharibi Dr. Anthony G. Mbassa
58. Biharamulo Mashariki Vedastus Lukumbuzya
59. Ngara Robson Robert Mushika
60. Mbeya Mjini. Joseph Mbilinyi.
61. Mbeya Vijijini Sambwee Shitambala
62. Mbarali Jidawa Hangwa Kazamoyo
63. Kyela Eddo Makata
64. Mbozi Magharb Silinde David.
65. Mbozi Mashark Mwampamba Mtela.
66. Rungwe Mash. Balton Gwakisa.
67. Rungwe Magh. Yusuph Asukile.
68. Karatu Israel Yohana Natse
69. Arumeru Magh. Martine Ole Kisambu
70. Arusha Mjini Godbless Lema.
71. Arumeru Mash. Joshua Samwel Nassari
72. Longido Paulina Laizer
73. Monduli Rev. Ole Silanga Mollel
74. Ngorongoro Moringe Lazaro Parkipunyi
75. Mpanda kati Said Arfi
76. Nkasi Kaskazini Keissy Salum Sood
77. Sumbawanga Mjini Veronika Salma Mwasa
78. Kwela Amir Nkulu
79. Kalambo Leonard Chilambo
80. Mpanda Magh. Daniel Masanja.
81. Nkasi Kusini Hypolito John Kaninga
82. Iramba Mash. Aaron Kikaya.
83. Singida Mash. Tundu A M. Lissu.
84. Singida Mjini Josephat Isango Hadu Nyimba
85. Iramba Magh. Mkumbo ndasi Shamdabula
86. Singida Kask. Msaghaa Omari Kimea.
87. Manyoni Mash. Musa Malecela
88. Manyoni Magh. Donald Madeje Lupaa
89. Singida Mash. Dr. Chritowaja Mtinda
90. Iringa Mjini. Rev. Peter Simon Msigwa
91. Njombe Kaskz. Alatanga Nyagawa.
92. Kalenga Eng. Ben Isdor Kihomwe
93. Makete Moses Klaunt Kyando
94. Kilolo Dr. Michael Mgatta
95. Njombe Magh. Thomas Nyimbo
96. Songea Mjini Adv. Edson Mboggoro
97. Mbinga Mash Boniface Ngonyani.
98. Peramiho Joseph Muhagama
99. Mbinga Magh. Cuthbert Ngwatta.
100. Tunduru kaskz Abdalah landi Daidi
101. Shinyanga Mjini Phillip Shelembi
102. Kisesa Erasto Tumbo
103. Kahama Charles Lubala
104. Msalala Edward Mlolwa
105. Meatu Meshakh Opurukwa
106. Kishapu Paulo Maghembe Kanogu
107. Bukombe Prof. Kulikoyela Kahigi.
108. Maswa Mash. Sylvesta Kasulumbayi
109. Bariadi Magh. Zacharia Thomas Makono
110. Bariadi Mash. Emmanuel Alphonce Kuchibanda
111. Maswa Magh. John Magale Shibuda
112. Kibakwe Benson Kigaila
113. Dodoma Mjini Enock Paulo Mhembano
114. Bahi Antoni Lyamunda.
115. Chilonwa Joel Mwaka
116. Kondoa Kaskz Abbas Kondo
117. Mtera John Lamecky Lubote
118. Mvomero Owden matokeo
119. Kilombero Regia Mtema
120. Morogoro Kusini Juma Abdul Tembo
121. Morogoro kusn mash Aquiline Magalambu
122. Morogoro Mjini Aman Mwaipaja
123. Kilosa Zainab Kisegere
124. Mikumi Onesmo Sambo Mwaikambo
125. Gairo Daniel Yustin Kambi
126. Ulanga Magh. Prof. Melchior Emeran Mlambiti
127. Korogwe Mjini Calistus Amiri Sheikbaha
128. Tanga Mjini Kassimu Amari Mbarak
129. Handeni Said Salehe Mbweto
130. Kilindi Pius Mseja Mbetta
131. Korogwe Vijijini Aaron Mashumve
132. Lushoto Deogratius Pio Kisandu
133. Mlalo Charles Kagonji.
134. Muheza Jumbe Said
135. Pangani Abdallah Mzee Omary
136. Kibaha Mjini Habib Mchange
137. Kibaha Vijijini Agnes Julius.
138. Mkuranga Sifa Majura
139. Chalinze Mustapha Baliche
140. Kisarawe Seleman Rajab Muhando
141. Mtwara Athumani Jeda Edwin
142. Masasi Moses Ambros Chiwanga
143. Newala Adam Sijaona Hangwanda
144. Lulindi Phanuel James Mhaiki
145. Tandahimba Rashid Abubakar matumla
146. Mtwara Vijijini AbdulRahman Said Sinani
147. Nachingwea Ali Omar Chitanda
148. Ruangwa Juma Khamis Lichonyo.
149. Lindi Mjini Samson Ali Nyagali
150. Mchinga Rashid Abdallah Njecherani.
151. Urambo Mashariki Msafiri Mtemelwa
152. Igalula Faraji Hussein Katalambula.
153. Nzega John Masanja Mezza.
154. Tabora kaskazini Subiri Salum mmeta
155. Tabora mjini Alhaji Jaji Musa Almasi Kikwima.
156. Bukene Dr. Joseph Buganga.
157. Igunga Fredrick David Kassita
158. Chumbani Mwanamrisho Abama
159. Magomeni Makame Salum Ali
160. Jang’ombe Maujani Salum Msabaha
161. Mtoni Yudith Theosil
162. Chwaka Ali Khamis Molid
163. Uzini Ali Mbarouk Mshimba
164. Bububu Yusuph Khatib
165. Mpendae Molid Hemed Khamis
166. Mkwajuni Haji Usihaji
167. Matemwe Posho Juma Kiboga
168. Ali Akalipo Ali Nungwa
169. Mfenesini Dhifa Mohamed Bakar
170. Bumbwini Mwadua Ali Khamis
171. Kiembesamaki Jumanne Shabani magazi
172. Chakechake Hafidhi Abdi Said
173. Chonga Salim Seif Nassor
174. Wawi Zainab Mussa baker
175. Mtambile Kombo M. Kombo
176. Kiwani Hassan Ame Kheir
177. Chambani Siti Ussi Shaibu
178. Mkoani Molid Nassor Said
179. Wete Molid Amour Abdallah
180. Kojani Salim Suleinman Said
181. Gando Hamed Mbarouk Mwinta,
182. Ole Sued Hamad Makame.

Tusikubali miaka mitano mingine ipotee

Evarist Chahali

MWAKA 2005 nilikuwa miongoni mwa waliokuwa na shaka juu ya uteuzi wa Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lakini baada ya ushindi wake wa kishindo, nilianza kuwa na imani naye, hasa kutokana na kauli zake za kuleta matumaini mapya.

Baada ya miaka 20 ya tawala za Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, nchi yetu ilihitaji mtu mwingine mwenye kuelewa kwa nini inazidi kuwa masikini wa kutupwa licha ya utajiri lukuki, mtu mwenye dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa kwa vitendo, si maneno matupu (kwa mfano kutangaza kuwa anawafahamu wala rushwa ila anawapa muda wa kijirekebisha).

Awali, sikuamini kuwa Kikwete angeweza kuipatia Tanzania kiongozi wanayemuhitaji kwa vile hukuwa na rekodi hiyo. Licha ya kwamba urais si taaluma inayosomewa, lakini uongozi bora unaweza kubashiriwa kutokana na rekodi ya nyuma ya kiongozi mtarajiwa hasa kwa vile kabla ya kuwa rais wetu, Kikwete alikwisha kushika nyadhifa kadhaa lakini pasipo rekodi ya kujivunia.

Hofu yangu kuhusu Kikwete ilianza kuyeyuka baada ya kusikia kauli yake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania ingekuwa kipaumbele chake kikuu pindi akichaguliwa, sambamba na kibwagizo cha Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.

Hotuba yake wakati anazindua Bunge, Dodoma, ilileta msisimko mpya, matumaini na imani kwamba hatimaye sasa tumepata kiongozi wa kuifikisha Tanzania inakopaswa kuelekea. Na hata alipotangaza baraza kubwa la mawaziri (lililojumuisha sura zenye utata), nado niliendelea kuwa na matumaini naye na kukubaliana na utetezi wake kwamba ili afanikiwe kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania angehitaji timu kubwa.

Matumaini yangu yalianza kufifia pale ulipotoa hotuba na kutamka kwamba “nawafahamu wala rushwa kwa majina lakini nawapa muda wa kujirekebisha”. Nilivunjwa moyo na kauli hiyo kwa sababu sijawahi kusikia mahala ambako rushwa ilikoma baada ya kiongozi kutoa muda kwa wala rushwa kujirekebisha. Na labda hapa niulize, hivi ile deadline aliyotoa mwaka 2006 kwa wala rushwa (aliodai kuwafahamu kwa majina) kujirekebisha bado haijaisha? Au ilikuwa indefinite deadline (isiyo na ukomo)?

Baadaye alirejea kauli kama hiyo alipofanya ziara ya ghafla Bandari ya Dar es Salaam alikotamka bayana kwamba anawafahamu wala rushwa katika sehemu hiyo na kilichobaki ni kuwaumbua tu (nadhani alimaanisha kilichobaki ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria). Inasikitisha kuona hadi leo hakuna aliyewajibishwa huku mamlaka husika zikirejesha mpira huo kwake kwa maelezo ya “waulizeni Ikulu maana wao ndio walidai wana orodha ya wala rushwa hapa”.

Tuwe wakweli, hivi kama aliahidi kuwasilisha majina ya mafisadi wa bandarini lakini hajatimiza ahadi hiyo maana yake ni nini? Je, tunastahili kuendelea naye kama ahadi alizotoa ni zisizotekelezwa? Kama anashindwa kutekeleza ahadi anazotoa mwenyewe pasipo kulazamishwa ataweza vipi kutekeleza mambo muhimu ambayo japo hajaahidi ni lazima ayatekeleze?

Ni kweli kwamba kiongozi wa nchi lazima afanye safari za kujitambulisha nje, lakini hicho hakiwezi kuwa ndiyo kipaumbele kwa kiongozi mwenye dhamira ya dhati ya kurekebisha hali ya nchi masikini kama yetu. Hata Barack Obama na David Cameron, viongozi wa mataifa tajiri kabisa duniani, wametuthibitishia kwamba kwenda nje ya nchi kujitambulisha si kipaumbele kwa kiongozi mpya.

Lakini pengine eneo tata zaidi ni la mafisadi. Kusita kupambana na kundi hili kumezua tafsiri nyingi katika vichwa vya watu, nyingi za hizo, hazimsemi vizuri Rais Kikwete kwa vile imejikita imani kwamba kuwaacha mafisadi waendelee ndiko kulikokwamisha “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania”.

Ni siri ya wazi kuwa aliingia madarakani kwa nguvu na jitihada za wanamtandao, wengi wao wakiwa watu wenye rekodi zisizopendeza. Kosa kubwa alilofanya ni kutotumia nafasi yake kama Rais kuwadhibiti, matokeo yake wameishia kuutumia urais wake kujinufaisha wao wenyewe.

Matukio mawili ambayo hayatafutika katika historia ya Urais wa Kikwete ni ujambazi wa fedha za EPA na utapeli wa kampuni ya Richmond na ‘binamu’ yake Dowans.

Kuhusu suala la EPA, wengi wetu tunaamini kwamba bado kuna maswali mengi kuliko majibu. Japo inapendeza kuwaona baadhi ya watuhumiwa wakifikishwa mahakamani, bado haieleweki kwa nini hadi muda huu wamiliki wa kampuni iliyokwiba fedha nyingi zaidi, Kagoda, wameendelea kuhifadhiwa.

Ni kweli safari hii pana ushindani wa kutosha kwenye kiti cha urais. Ni kweli pia kwamba kama akipita, Kikwete atakuwa, kwa mujibu wa Katiba, akitumikia kwa muhula wake wa mwisho. Ninachojiuliza ni kama amemudu kufumbia uoza wote huu katika kipindi muhula wake wa kwanza huku akijua fika kuwa baada ya miaka mitano angepaswa kuomba tena ridhaa ya kupigiwa kura, hali itakuwaje katika muhula wake wa mwisho ambao hatahitaji tena kura zetu?



Barua-pepe:
epgc2@yahoo.co.uk

CHADEMA YAFUNIKA MJI WA ARUSHA

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15816&d=1288241646

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15817&d=1288241863

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15818&d=1288242109

MKUTANO WA CHADEMA UNGA LIMITED ARUSHA

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15819&d=1288242331

Wednesday, October 27, 2010

FREEMAN MBOWE AITIKISA ARUSHA

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15795&d=1288191611

UMATI ULIOKUWA UNAMNGOJA MWENYEKITI YA CHADEMA FREEMAN MBOWE

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15796&d=1288191627

DR SLAA ALIVYOTIKISA MWEMBEYANGA

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni leo mchana.
Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo jioni.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke leo jioni.Picha kwa hisani ya Joseph Senga wa Tanzania Daima.

Tuesday, October 26, 2010

CD ZA MDAHALO WA DR SLAA

Napenda kuwajulisha kwamba CD za Mdahalo wa DR W P Slaa sasa ziko Tayari kwa ambaye atakuwa anazitaka anaweza kupiga namba 0766 334049 au tuma email kwenda friendsofslaa@gmail.com Gharama yake ni shilingi Alfu 10

Unaweza kutumiwa popote ulipo Tanzania

kataeni kushawishiwa ama kuhusishwa katika fujo au vurugu-igp mwema.

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Said Mwema amewaomba wananchi kuwa na ushirikiano katika kukataa kushawishiwa ama kuhusishwa katika uvumi, fujo au vurugu zozote zinazoweza kuingiza nchi kwenye machafuko yasiyo ya maana yoyote.

Aidha Mkuu huyo , amesema kuwa amani na usalama na utulivu hapa nchini vitadumishwa wakati wote kabla na baada ya uchaguzi, kwa kuhakikisha kwamba sheria , kanuni na taratibu za nchi zinafuatwa ipasavyo.

“Tukumbuke kwamba vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa sheria, kabla na baada ya uchaguzi ni uhalifu.Sheria haina udhuru, inachukua mkondo wake mara moja endapo ukiukwaji umefanyika. Hivyo kutii sheria na taratibu za uchaguzi ni wajibu wa kila mpiga kura na kila mwananchi,” alisema Mwema.

Aliongeza kuwa baada ya kura kupigwa na zoezi hilo kufungwa rasmi, hatua inayofuata ni kuzichambua na kuzihesabu ili kupata matokeo, hivyo huo ndo wakati wananchi wanatakiwa kuwa na subira, kwa sababu zoezi hilo ni muhimu na linapaswa kuendeshwa kwa umakini wa hali ya juu ili, haki itendeke na kuepusha malalamiko.

Mkuu huyo alisema baada ya matokeo kutangazwa ni muhimu kutambua kwamba aliyeshinda ndiye aliyepigiwa kura nyingi na watu wengi.

“Wote tunawajibu wa kumkubali , kumtambua na kushirikiana naye ili kumsaidia kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa watu wote,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarouk Abdulwakil aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi au udini kuendelea kuwa na msukumo wa utaifa na kuacha maslahi binafsi ili amani, usalama na utulivu vidumu kabla ya baada ya uchaguzi.

Alisema wizara yake inawahakikishia wananchi kwamba nchi itakuwa katika hali ya amani, usalama na utulivu wakati wote huku, hivyo alisisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi .

CHAGUA CHADEMA CHAGUA SAID AMOUR ARFI MPANDA

Mgombea ubunge Bw Said Amour Arafi ambaye pia ni makamu mwenyekiti Taifa Chadema akiwa katika ukumbi wa mdahalo ukumbi wa Katavi mjini Mpanda

CHAGUA CHADEMA CHAGUA KEISSY SALUM SOOD NKASI KASKAZINI

Mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Nkasi KaskazinI Bw Keissy Salum Sood

DR SLAA AUNGURUMA MANZESE

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15746&d=1288096234

Mkutano wa DR W P SLAA LIVE TOKA MwembeYanga

Nawakaribisha katika mkutano wa Mgombea uraisi kwa tiketi ya chadema DR W P SLAA unaofanyika hapa Kwenye uwanja wa Mwembe yanga watu wamejaa kweli kweli , kumefurika na kutia fora – Kuna watu wa aina mbalimbali hapa kuanzia wazee , vijana na wale watu wakati , kuanzia wamachinga mpaka wauza mitumba walioacha biashara zao kwa muda kwa ajili ya kuja kumwona dr slaa akinadi sera zake uwanjani hapa

Kwa wale walio mbali na maeneo haya wanafuatilia mkutano huu wanaweza kutazama TC1 Kuanzia saa 9 Kamili , wengine wanaweza kufuatilia kwa njia ya mtandao kama hii .

Kwa wale wanaopenda kuchangia Kampeni hizi wanaweza kutembelea blogu yetu kwa anuani www.marafikiwaslaa.blogspot.com kama una habari zaidi unaweza kututumia kupitia friendsofslaa@gmail.com

Wale wanaopenda kuchangia mkakati wa kutengeneza vipindi vya TV vinavyoendelea kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya TV na radio wanaweza kuchangia kupitia namba

+255766334049 MPESA
+255786806028 ZAP

Kama unataka Fulana za DR SLaa na Kofia zenye sahihi yake wasiliana na 0714 667026

dk slaa alivyounguruma zanzibar

Mgombea Urais kwa chama cha CHADEMA Dk Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wake wa kampeni wa lala salama, uliofanyika katika viwanja vya Garagaza,vilivypo Mtoni, Unguja, Zanzibar. (Picha na Emmanuel Herman).

Monday, October 25, 2010

Slaa kuunguruma Mwembeyanga

Napenda kuwafahamisha kuwa kesho Dr. Slaa atakuwa viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa LIVE ndani ya TBC1 pia kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa masaa 3.

Aidha, baadae atakuwa LIVE katika televisheni ya Agape kuanzia saa 1 jioni.

Mkutano wake leo umejaza watu wengi sana huko Zanzibar tofauti na wengi mnavyoweza kudhani, nitawaletea picha za Zanzibar hali ilivyokuwa.

DR SLAA AUNGURUMA ZANZIBAR


NUKUU ZA DR WP SLAA


  1. Monduli wanaishi maisha magumu.
  2. Tanzania bila CCM inawezekana, na kuendelea kukaa na CCM ni maafa makubwa.
  3. Kama ningesema uongo kuhusu ufisadi wa JK na waswaiba wake, mbona sichukuliwi hatua?
  4. Ukitukanwa, angalia, puuzia na uondoke. Ukipigwa kofi, mgeuzie na la pili...!
  5. Sipendi kwenda ikulu huku damu zikimwagwa, au kuwaacha watanzania wakiwa vilema kwa ajili yangu...!
  6. Nipo tayari kula mihogo ikulu, ili mtoto wa tanzania asome...!
  7. Siendi kuwa raisi wa Afrika Mashariki, bali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...!
  8. Kodi ya saruji kutoka Tanzania ni 18%, Kenya 15% na Uganda 16%....! Eti ndio makubaliano yaliyowekeana kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki...!
  9. Ninazo nyaraka kuwa serikali ya Tanzania imefanya partial payments huko Canada kwa ajili ya mabango ya CCM...!
  10. Sikatai kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini lazima tufanye maandalizi kuwapatia watanzania elimu itakayowawezesha kuingia kwenye ushindani...!

CHAGUA CHADEMA CHANGIA CHADEMA

Wakazi wa Kawe waliojitokeza kwa wingi leo jioni kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,Dk Slaa katika kampeni zake za lala salama.


Wakazi wa Kawe wakiwa katika viwanja vya Tanganyika Pekaz

Maelfu ya wakazi wa Kawe waliojitokeza