Sunday, February 13, 2011

Wabunge wa CHADEMA Wazindua Matawi vyuo Vikuu

Jana siku ya Jumamosi tarehe 12 Februari 2011 kwa nyakati tofauti Wabunge wa CHADEMA wamezindua matawi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Mt Johns na Mipango.Kabla ya Uzinduzi kulitanguliwa na hotuba fupi fupi za wabunge hao. Mikutano yote ilikuwa ni mizuri sana.

Wabunge waliowakilisha Chama ni

1. Prof Kahigi- Bukombe
2.Halima Mdee- Kawe
3.John Mnyika-Ubungo
4.Godbless Lema-Arusha Mjini
5.Rebecca Mgodo-Viti Maalum Arusha
6.Regia Mtema- Vitimaalum Kilombero

Wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo Cha Mt John wamejiunga na CHADEMA sambamba na ufunguzi wa ofisi ya tawi hilo.

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa Vyuo vya Mipango na UDOM wamejiunga na CHADEMA Sambamba na ufunguzi wa Tawi.


Wabunge hawa walipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanafunzi hao.

Mapambano yanaendelea,Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

0 comments:

Post a Comment