Friday, February 11, 2011

Upotoshaji wa Kauli ya Mhe FreeMan Mbowe Bungeni

Nimeandika hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umefanyika hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge.Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema.Kuongeza ni suala la kawaida sana.Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali.Hansard ikitoka nitaweka hapa.

REGIA MTEMA

0 comments:

Post a Comment