Sunday, February 27, 2011

CHADEMA Kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa

Baada ya kuingia Musoma na kufanikiwa kufanya maandamano kwa amani na utulivu mkubwa leo vikosi vitatembelea Wilaya za Mkoa huu. Lakini kabla ya kwenda kwenye wilaya, Viongozi wote tukiongozwa na Kamanda Mbowe tutaelekea kuzuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuweka mashada ya maua.

Vikosi leo vitaelekea Tarime, Rorya, Bunda, Serengeti, Mwibara na Musoma Vijijini.

Hauna Kulala Mpaka Kieleweke.

0 comments:

Post a Comment