Nimekuwa nikifuatilia sana TBC1 katika taarifa zao za habari kila saa 2 ya
usiku.na nimekuwa ninavutiwa sana na TBC1 kwa jinsi ilivyofanikiwa kuwavutia
watanzania kwa style yake ya taarifa ya habari ambayo haitofautiani na
mashirika makubwa ya habari ya kimataifa kama BBC,CNN,EL-JAZEERA n.k.,pia
nimekuwa nikivutiwa na division of labour/specialization iliyoko TBC1.Kuna
watangazaji ambao wao ni taarifa ya habari tu,na kuna wengine wao ni USIKU
WA HABARI tu nakadhalika na kadhalika.Pia TBC1 ya sasa sio ile ya akina enzi
za mwaffisi,ya sasa ni ya kisasa kabisa,isiyoegemea chama chochote,mfumo
wowote,itikadi yoyote nakadhalika.Kuna kitu kinachonishangaza
kidogo.kurushwa kwa habari za CHADEMA hasa mgombea urais wa CHADEMA.Siku ya
kwanza kabisa Dr.Slaa alipokwenda karatu kuwaeleza wapiga kura wake uamuzi
wake wa kuacha kugombea ubunge na kugombea urais,TBC1 katika taarifa yake ya
habari ya saa 2 usiku hawakuuonyesha mkutano huo wa hadhara huko
karatu.naninavyojua TBC1 ina waandishi wanaotuma habari muda huo huo
wakati tukio
linaendelea,au muda mfupi kabisa baada ya tukio kwisha,lakini habari za
mkutano niliziona kesho yake asubui ktk habari ya saa 1 asubui siku
iliyofuata.sasa nikajiuliza,ni wangapi wanaangalia habari ya saa 1
asubui?watu wengi muda huo ndo wanakuwa wanaelekea makazini na kupambana na
foleni za jiji la dar.mimi nadhani ni mbinu chafu ambayo CHADEMA imeandaliwa
ili kupunguza moto uliowashwa wa mageuzi nchini.watu wamejiandaa kuangalia
taarifa ya habari ya saa 2 usiku,then habari hairushwi muda huo inapelekwa
asubui ya siku inayofuata.pia,habari za CHADEMA zinachukuwa muda mfupi sana
kuongelewa na mtangazaji wa habari.niwaulize TBC1,JE KULIKONI NA CHADEMA??!!
Funga kazi ilikuwa ni mkutano wa Dr.Slaa leo tarehe 7/8/2010 katika jiji la
dar es salaam.kwanza kapewa muda kidogo kabisa,na CHA AJABU,TBC1
HAWAKUONYESHA HATA UMATI WA WATU WALIOKUWA WAKIMSIKILIZA
DR.SLAA.Wamemuonyesha slaa tu kwa juu (kuanzia kiunoni kwenda juu) ili hata
watu wasionyeshwe angalau vichwa vyao tu tujue kama kulikuwa na idadi kubwa
ya watu.Lakini ngoja niseme..kila jambo na wakati wake (Mhubiri 3),kuna
wakati wa masika na wakati wa kiangazi,wakati wa kulia na wakati wa
kufurahia,wakati wa majonzi na wakati wa shangwe, n.k.,WAKATI WA KUSHANGILIA
UMEFIKA,MAJONZI TUTAYAWEKA PEMBENI VERY SOON.majira ya kufanya kazi kwa
interest ya chama fulani au serikali furani pia yatakwisha tuuuu!!MOTO
UMEWASHWA HATA KAMA WATAINYIMA CHADEMA COVERAGE,HATA KAMA COVERAGE NI YA
SEKUNDE 5,NO PROBLEM!! WAKATI WA MAGEUZI UMEFIKA,WAKATI WA USHABIKI
UMEKWISHA,NI WAKATI WA FACTS.NI WAKATI WA KUTETEA NA KUPIGANIA MASLAHI NA
MAISHA BORA YA MTANZANIA,SI WAKATI TENA WA KUJIPENDEKEZA.MUDA
UMEWATUPA,UNAWAACHA,WATALIA NA KUSAGA MENO PALE WANANCHI WATAKAPOSEMA ENOUGH
IS ENOUGH,TUNATAKA MAGEUZI YA UCHUMI NA MAENDELEO KWA UJUMLA.
MUNGU SI MWANADAMU ASEME UONGO (Hesabu 23:19)!
mwanamageuzi,
MJADALA ZAIDI HAPA TBC1 NA AJENDA YA SIRI DHIDI YA DR.SLAA NA CHADEMA KWA UJUMLA
Dira Ya Dunia
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment