Kwa kawaida vituko, kashfa, rushwa na mizengwe kwenye chaguzi zaTanzania imekuwa ni kawaida. Mara nyingi yule anayeweza kucheza siasaza rafu kwenye chaguzi za ndani ya CCM yeye ndio huibuka mshindi.Kwahiyo kwa wale wasioweza rafu, wanaoamini kwenye uadilifu na ukwelikwao kuweza kuongoza kupitia chama tawala ni kitu ambacho hakiwezekaniau ni kigumu saaana. Sina hakika km yupo/wapo wana CCM ambaowamepitishwa kwenye chaguzi zao bila kufanya mizengwe hata kidogo.Matokeo yakitangazwa kwenye chaguzi hizo, mambo mengi hujitokeza.Wengine huamua kuunda makundi na kimya kimya kuunga mkono wagombea waupinzani na wengine huamua kuhama chama kabisa. Na hapa ndio kwenyemjadala.Hivi karibuni wagombea wengi wa CCM wamelalamikia kuchezewa rafu nawengine kuahidi kuhama vyama. Na hii sio mara ya kwanza wapo wengihuko nyuma waliowahi kufanya hivyo km mh Njelu Kasaka, (CCM-CUF-CCM)na wengineo. Lakini pia suali la msingi la kujiuliza, linabaki ninihasa lengo la vyama vya upinzani??? Je, lengo ni kuwa na uwakilishimkubwa bila kujali aina ya watu waliopo upinzani au lengo ni kukidhihaja ya maendeleo ya Watanzania? Km lengo ni kuleta maendeleo kwaWatanzania basi lengo hilo linakinzana na aina ya watu wanaohamiakwenye vyama hivi si kwa sababu ya sera za upinzani bali ni kwa sababuwanadhani wanawaadhibu chama Tawala.kwa mtindo huu, je kuna dhamira ya dhati kutoka kwa baadhi yaWatanzania wenzetu kujikomboa katika ufisadi na umasikini uliokithiri??
FUATILIA MJADALA HUU HAPA Je Wapinzani Wanadhamira Ya Kutukomboa ?
Dira Ya Dunia
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment