Showing posts with label PICHA/PICTURES. Show all posts
Showing posts with label PICHA/PICTURES. Show all posts
Saturday, March 5, 2011
Tuesday, March 1, 2011
Thursday, February 24, 2011
Monday, February 21, 2011
Dk Wilbrod Slaa Ashiriki Kwenye Misa Ya Watu wa Tatu Wa Familia Moja Waliofariji Kwa Ajali ya Mabomu Gongo la Mboto
Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Willibrod Slaa akiwa na Mke wake kwenye mazishi ya mama na watoto wake wawili kutoka familia moja ya Jacob Nyajengo wa Mzambarauni,waliokufa kwa kuangukiwa na nyumba ya jirani, kutokana mabomu yaliyolipuka kutoka ghala la Silaha katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo la Mboto,Dar es Salaam.Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alifuatana pia na wabunge kadhaa kwa tiketi ya chama hicho.Picha hii na Mdau Bashir Nkromo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na Mbunge wa Singida Mashariki-Chadema Mheshimiwa Tundu Lissu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia)akiteta jambo bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki-Chadema Mheshimiwa Tundu Lissu bungeni
Tuesday, February 15, 2011
UZINDUZI WA TAWI LA CHADEMA CHUO CHA MIPANGO DODOMA
Mgeni rasmi ktk uzinduzi wa tawi hilo mbunge viti malumu(MBEYA)Mheshimiwa Naomi Kaihula akiongea baada ya uzinduzi kushoto kwake ni mbunge wa arusha Godless Lema kutoka Chadema
Mbunge wa Kawe -Chadema Mheshimiwa Halima Mdee akiunguruma kwenye mkutano huo
Mbunge wa Ubungo-CHADEMA Mheshimiwa John Mnyika akinguruma katika Mkutano huo
Mbunge wa viti maalumu Arusha mjini (CHADEMA) Mheshimiwa Rebecca Michael Mngodo akiongea
wanachama wa CHADEMA tawi la chuo cha mipango DODOMA wakishangiria ktk uzinduzi wa Ofisi ya CHADEMA eneo la MIYUJI Dodoma, ofisi hiii ya tawi la chadema eneo la miyuji imefunguliwa rasmi February 12-2-2011 na mbunge wa viti maaalum chadema mkoani mbeya Mheshimiwa Naomi Kaihula na kuhudhuriwa na Wabunge wa chadema ambao wapo kwenye shughuli mbalimbaliz a vikao vya bunge mjini dodoma
Sunday, February 13, 2011
Wabunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA
Wabunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA,Naomi Mwakyoma (Mbeya), kushoto, na Rebeca Mngodo ( Arusha) wakifuatilia kwa makini mkutano
Friday, February 11, 2011
Mbunge wa Singida Mjini Mohammed Dewji (kulia) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe
Mbunge wa Singida Mjini Mohammed Dewji (kulia) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe wakijadiliana jambo katika viwanja vya Bunge Dodoma.
Wednesday, February 9, 2011
CHADEMA NA VIONGOZI WAKITOKA NJE
KAMBI YA UPINZANI Bungeni
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe(kushoto)akiongoza Wabunge wa Chadema kutoka Ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe
Wabunge wa Chadema Wakitoka Ndani ya Ukumbi wa Bunge Jana Jioni.Picha Zote na Mwanakombo Juma-MAELEZO
Tuesday, February 8, 2011
Wabunge wakitafakari kuhusu muhtasari uliotolewa
Wabunge wakitafakari kuhusu muhtasari uliotolewa mara kabla ya wasaa wa kuuliza maswali.Picha na Prosper Minja-Bunge
Monday, February 7, 2011
MH FREEMAN MBOWE AKISALIMIANA NA MHE JAKAYA KIKWETE
Sunday, January 30, 2011
Monday, January 24, 2011
MAANDAMANO YA CHADEMA DODOMA
Maandamano ya Jumamosi Dodoma yalikuwa mazuri. shukurani za pekee kwa jumuiya ya wana UDOM kwa kujitokeza kuyapamba. maandamano haya yalitokea ofisi za mkoa Dodoma, yakaenda hadi soko la Majengo, yakapita independence square, hadi stand ya mkoa...toka hapo yakaelekea njia ya bungeni hadi CBE na kushika barabara ya makole. Yakanyoosha moja kwa moja hadi viwanja vya barafu.
Mkurugenzi wa organaizesheni Ben Kigaila ndiye aliyaongoza na ndiye aliyepokea tamko na kuhutubia. pamoja naye wagombea mbali mbali waliochakachuliwa na kiongozi wa wanafunzi wa udom waliopata nafasi ya kuzungumza na wananchi. Sam Kigaila naye akapewa nafasi ya kuzungumza...Sam ni soo!! sisiemu lazima wamejifunza kuwa hawataweza kuzuia nguvu ya umma kwa kumuangamiza Slaa kwani kuna topaz za uhakika nyuma yake....
Katibu wa mkoa aliweza kutamka rasmi kuwa polisi vihiyo mfano aliyekuwa karani wa mahita akipata cheo ndio mwanzo wa shida. inasemekana wakati maandamano yanaendelea mashuzi yaliwatoka wana ccm na kumpigia RPC kumuuliza kwanini ameruhusu maandamano. Naye aliwajibu kuwa ni ya amani. Polisi waliongoza maandamano yooote kwa uzuri.
Baada ya hapo kamanda kigaila alionana alifungua tawi la chadema kata ya uhuru, akapata kuzungumza na halafu akaonana na wanachadema tawi la UDOM ambao walimueleza mengi yakiwamo manyanyaso wanayofanyiwa na baadhi ya walimu kwa kuwa tu ni wanachadema. Aliahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo..
Baada ya hapo akaenda george town miyuji kuonana na wanafunzi wa chuo cha mipango. akiwa huko alionuyeshwa orodha ya papo kwa papo ya wanafunzi 300 ambao wanatyaka kadi. alihakikishiwa kuwa asilima 95 % ni wana chadema. Uongozi wa muda ulichaguliwa na kuambiwa utafute ofisi na uendelee kuandikisha wanachama. Mheshimiwa Mbowe atakuja kuzindua tawi na kukabidhi kadi..
Wakiwa na wanachuo hao wa mipango, mhenshimiwa dada kunti ambaye ni diwani aliyechakachuliwa wa ipagala aliwataka wanafunzi kuhimiza wanawake na kuanzia magirlfriend wao kuingia CHADEMA kwani ndio tofali lililobaki. Alisisitiza kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kukinyanyua chama...
Picha za mwisho zinamwonyesha kijana akisimika bendera nyumbani mwa kweleakwelea!
Natuma picha hizi kubatilisha uwongo wa TBCCM kuwa maandamano hayakupata kibali cha wananchi na yalihudhuriwa na watu wachache!
Vyombo vya habari, kazi kwenu!
Naomba kuwasilisha!