Watanzania wasiotaka mabadiliko na maendeleo kwa nchi yao wataichagua CCM, lakini ikumbukwe kuwa ni hiyohiyo CCM iliyotufikisha hapa kwenye umasikini huu mkubwa tulionao. Ni hawahawa walioshindwa kudhibiti mfumuko wa bei. Ndio hawahawa wanaotuletea uchungu na shida katika nchi yetu wenyewe. Wakoloni Weusi, ndugu zetu,jamaa na rafiki zetu wa tangu udogoni.Wananchitwendeni tukapige Kura kisha tuzilinde kura hizo dhidi ya madhalimu. Tusikae jirani ya vituo vya kupigia kura ila mbali na eneo la kupigia kura na kuchukua tahadhari kwa yeyote atakayekwenda eneo la kuhesabia kura baada ya muda wa mwisho wa kupiga kura hasa kipindi cha kuhesabu kura hizo. Najua Polisi watamwagwa kuhakikisha mmerudi majumbani nafasi ambayo wataitaka sana, jigaweni katika zamu zenu kulinda haki yenu mpaka kieleweke, msiamini mawakala pekee nao ni binadamu, kila mmoja awe mlinzi wa kura yake. Je wataweza kutuhonga sote?
Kama kuumia kwa miaka mingine mitano tutaumia sote na kizazi chetu. Tusifanye makosa tena
Dira Ya Dunia
27 minutes ago
0 comments:
Post a Comment