Wednesday, January 12, 2011

Maandamano ya CHADEMA Mara

12th January 11
Chadema Mara yaitisha maandamano Jumamosi

George Marato
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, kimeitisha maandamano makubwa utakaohusisha mkoa mzima kupinga kile walichokiita vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za raia vilivyofanywa na Jeshi la Polisi mjini Arusha.
Kwa mujibu wa Chadema Mkoa wa Mara, maandamano hayo yatalenga kupeleka ujumbe kwa taifa na dunia kulaani vikali hatua ya jeshi hilo kutumia nguvu kubwa, ikiwamo risasi za moto na mabomu ya machozi kuzima maandamano yaliotishwa na chama hicho hivi karibuni mjini humo.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Nyanza Sibitali, aliliambia Nipashe mjini hapa kuwa maandamano hayo yatafanyika Jumamosi wiki hii yatakayohusisha majimbo saba ya uchaguzi ya mkoa wa Mara na kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kupeleka ujumbe huo.
Alisema Mkuu wa Mkoa ndiye anayetarajia kupokea maandamano hayo kisha kupokea ujumbe huo ingawa alisema bado hawajampata mkuu huyo wa mkoa kumweleza uamuzi huo.


NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/fun...le.php?l=25011

0 comments:

Post a Comment