Saturday, January 15, 2011

KONGAMANO LA KATIBA UDSM

Waendeshaji wa Mdaharo wa kujadili swala la Katiba mpya ya Tanzania kwa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA),toka kushoto ni Prof. Issa Shivji,Dr. Kitila Mkumbo pamona ja Ndg. Jenerali Ulimwengu wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa mdaharo huo mchana huu katika ukumbi wa Nkurumah,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ndg. Jenerali Ulimwengu akizungumza katika mdaharo huo ambao ulikuwa na changamoto nyingi kutokana na mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Prof. Issa Shivji azungumza katika Mdaharo huo huku akinukuu baadhi ya maneno yaliyokuwa yakitamkwa na Hayati Mwl. Nyerere kuhusiana na swala la Katiba Mpya.Mdaharo huu umemalizika hivi punde katika ukumbi wa Nkurumah ulipo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mchana huu.
Mmoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Mzee Ibrahim Kaduma akichangia mada zilizokuwa zikutolewa na baadhi ya wajumbe waliohudhulia Mdaharo huo kuhisia na swala la kupatikana kwa Katiba mpya ya nchi yetu.Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake nchini (TAMWA),Mama Ananilea Nkya akichangia mada katika Kongamano hilo.
Mmoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada.
Baadhi ya Wanataaluma na wanasiasa wakongwe wakifuatilia Mdaharo huo.
Kila mmoja alikuwa akitaka kuchangia jambo katika Mdaharo huo uliomalizika hivi punde katika ukumbi wa Nkurumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ukumbi ukiwa umefurika kusikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na wajumbe mbali mbali katika mdaharo huo.
source : issamichuzi

0 comments:

Post a Comment