Monday, January 24, 2011

MAANDAMANO YA CHADEMA DODOMA

Maandamano ya Jumamosi Dodoma yalikuwa mazuri. shukurani za pekee kwa jumuiya ya wana UDOM kwa kujitokeza kuyapamba. maandamano haya yalitokea ofisi za mkoa Dodoma, yakaenda hadi soko la Majengo, yakapita independence square, hadi stand ya mkoa...toka hapo yakaelekea njia ya bungeni hadi CBE na kushika barabara ya makole. Yakanyoosha moja kwa moja hadi viwanja vya barafu.

Mkurugenzi wa organaizesheni Ben Kigaila ndiye aliyaongoza na ndiye aliyepokea tamko na kuhutubia. pamoja naye wagombea mbali mbali waliochakachuliwa na kiongozi wa wanafunzi wa udom waliopata nafasi ya kuzungumza na wananchi. Sam Kigaila naye akapewa nafasi ya kuzungumza...Sam ni soo!! sisiemu lazima wamejifunza kuwa hawataweza kuzuia nguvu ya umma kwa kumuangamiza Slaa kwani kuna topaz za uhakika nyuma yake....

Katibu wa mkoa aliweza kutamka rasmi kuwa polisi vihiyo mfano aliyekuwa karani wa mahita akipata cheo ndio mwanzo wa shida. inasemekana wakati maandamano yanaendelea mashuzi yaliwatoka wana ccm na kumpigia RPC kumuuliza kwanini ameruhusu maandamano. Naye aliwajibu kuwa ni ya amani. Polisi waliongoza maandamano yooote kwa uzuri.

Baada ya hapo kamanda kigaila alionana alifungua tawi la chadema kata ya uhuru, akapata kuzungumza na halafu akaonana na wanachadema tawi la UDOM ambao walimueleza mengi yakiwamo manyanyaso wanayofanyiwa na baadhi ya walimu kwa kuwa tu ni wanachadema. Aliahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo..

Baada ya hapo akaenda george town miyuji kuonana na wanafunzi wa chuo cha mipango. akiwa huko alionuyeshwa orodha ya papo kwa papo ya wanafunzi 300 ambao wanatyaka kadi. alihakikishiwa kuwa asilima 95 % ni wana chadema. Uongozi wa muda ulichaguliwa na kuambiwa utafute ofisi na uendelee kuandikisha wanachama. Mheshimiwa Mbowe atakuja kuzindua tawi na kukabidhi kadi..

Wakiwa na wanachuo hao wa mipango, mhenshimiwa dada kunti ambaye ni diwani aliyechakachuliwa wa ipagala aliwataka wanafunzi kuhimiza wanawake na kuanzia magirlfriend wao kuingia CHADEMA kwani ndio tofali lililobaki. Alisisitiza kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kukinyanyua chama...

Picha za mwisho zinamwonyesha kijana akisimika bendera nyumbani mwa kweleakwelea!

Natuma picha hizi kubatilisha uwongo wa TBCCM kuwa maandamano hayakupata kibali cha wananchi na yalihudhuriwa na watu wachache!

Vyombo vya habari, kazi kwenu!

Naomba kuwasilisha!0 comments:

Post a Comment