Sunday, October 31, 2010

HABARI/TAARIFA ZA UCHAGUZI TANZANIA 2010

Matokeo yaanza kutangazwa

Matokeo yaanza kutangazwa - ZANZIBAR/PEMBA

TUME YA UCHAGUZI IMEBORONGA

NAMBA ZA MAKAO MAKUU CHADEMA

01: Mbogo: 0683-179001, 0714-776673
02: Mahinda: 0715-949019
03: Dady Igogo: 0713-616096
04: John Mnyika: 0754-694553

Fuatilia mwenendo kwa kugonga


Taarifa / Habari za Uchaguzi Mkuu - Upigaji Kura

State of the Nation Report 31st October 2010

www.wanabidii.net


Saturday, October 30, 2010

Mbinu zinazoweza Kutumika Kuiba Kura

Zifuatazo ni mbinu zitakazotumika kuiba kura kesho na zimeanza kutumika mkoani Shinyanga!!!

1.0 Mabalozi wote wa nyumba 10 na viongozi wa serekali za mitaa wanaitwa, wanapewa karatasi 2 za kupigia kura zilizo na vema tayari kwa mgombea wa kijani. Karatasi moja ni ya mume na moja ni ya mke wake. Kesho kila mmoja atakapoingia chumba cha kupiga kura atatakiwa achukue karatasi ingine (ya awali atakuwa kaificha). Akisha piga kura, atadumbukiza kwenye sanduku karatasi zote mbili. Hivyo mjumbe mmoja atapiga kura 2 na mkewe/mumewe kura 2. Jumla 4

Chadema wafanyeje kudhibiti hali hii??? Waweke daftari ambalo kila anaeingia anaandika namba kuanzia 1 hadi mtu wa mwisho. Baada ya kuhesabu kura, zitakazozidi zitakuwa ni zile zilizochakachuliwa!!!!!

Kama itawezekana, kila mpiga kura akaguliwe idadi ya karatasi atakazotumbukiza kwenye sanduku la kupigia kura. Else, wawakague watu kabla hawajawapa karatasi za kupigia kura, kujiridhisha kwamba, hawana vibomu/videsa vya ziada.

Its serious vikao vinaendelea kutimiza azma ya kupiga kura kwa design hiyo, japo maeneo yaliyolengwa ni yale yenye upinzani wa kweli. Mf. Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mwanza na Mara. DSM inaogopwa sababu ya mwamko na kusambaa kwa taarifa sababu ya teknologia!!

2. Mbinu ya pili ni kutoa karatasi za kupigia kura zisizo na muhuri sambamba na zenye muhuri wa tume ya uchaguzi, ambapo karatasi zisizokuwa na muhuri zitachukuliwa kuwa batili kwa sababu hazijapigwa muhuri wa NEC.

Chadema wafanye nini hapa!!! Kila mtu anapofika kupiga kura, mawakala wapitie kila karatasi anayopewa mpiga kura kuhakikisha kwamba karatasi anayopewa mpiga kura ina muhuri sahihi.

3. Kuchakachua kura zikiwa njiani kwenda kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo!!! Kwenye sheria za NEC na taratibu za internal control (Sarbanese Oxley Act), hapa kuna leakage. Hakuna anaeweza kuthibitisha kuto kuchakachuliwa kwa masanduku ya kura njiani kwakuwa mawakala hawana uwezo kusindikiza kura hizo!!!

Naomba kuwashirikisha mbinu hizo chafu kutokea Shinyanga!!! Hali si hali

Mungu awalinde na kuwabariki, awawezeshe nyote kupiga kura kwa umakini na kwa amani na kumpata Raisi wa kutuongoza kwa kipindi kijacho cha miaka mi tano mwenye hekima, akili, busara na hofu ya Mungu ndani yake!!!

Kampeni ya Mwisho ya DR W P SLAA Mkoani Mbeya








Amri kumi za Uchaguzi

1. Tambua kwamba kura ni silaha takatifu inayokuwezesha kumchagua yule
unayeamini kwamba unaweza kumkabidhi sehemu ya maisha yako na ukawa salama.
Tumia busara.

2. Jua kwamba ni usaliti kwako mwenyewe na kwa wananchi wengine iwapo
utapiga kura kwa misingi ya rushwa. Anayekununua hakuthamini. Kwake wewe ni
bidhaa tu, kama maharage.

3. Usiruhusu hisia za ubaguzi wa kabila, rangi, dini, jinsia, au ubaguzi wa
aina yoyote nyingine ili utawale uamuzi wako katika kupiga kura.

4. Tenda haki kwa wengine, na pia dai haki yako kutoka kwa wengine.
Usimwonee yeyote na wala usimruhusu yeyote akuonee.

5. Watetee na walinde wanyonge na wasiojiweza. Wasaidie ili waweze kutumia
haki yao ya kupiga kura.

6. Imarisha uhuru wako na uhuru wa nchi yako kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi
unakuwa na maana, na kwamba kila kura inayopigwa ina maana.

7. Epuka vurugu, vitisho na ugomvi. Kura ni jambo la raha, si karaha.

8. Kumbuka kwamba amani ni mwana wa haki. Penye haki, aliyeshindwa akubali
kushindwa, na aliyeshinda bado atende haki kwa aliyeshindwa.

9. Tambua kwamba uchaguzi unakuja na kwisha, viongozi huja na kuondoka,
lakini Taifa na watu wake hudumu milele. Tuliza hamasa, epuka chuki, uwe na
ustahimilivu.

10. Hii ni fursa adhimu; ifurahie.

JENERALI ULIMWENGU

Kipindi maalumu kwenye ITV na Dk Slaa (Saa 9.30 hadi Saa 10.30)

Kutakuwa na kipindi maalumu cha Dk Slaa katika ITV leo siku ya mwisho wa kampeni kuanzia saa 9.30 hadi saa 10.30 jioni. Katika kipindi hiki Dk Slaa atafanya majumuisho ya kampeni zake na kuwaomba tena watanzania wamchague hiyo kesho.

Awali kipindi hiki kilikuwa kirushwe kuanzia saa 11 hadi saa 12, lakini katika hali ya kushangaza, ghafla ITV wameomba radhi kwamba kipindi hiki hakiwezi kuonyeshwa katika muda uliokubaliwa awali. Habari zilizopo ni kwamba CCM wakiongozwa na Kinana wameenda leo asubuhi kuwaomba ITV wasionyeshe hicho kipindi katika muda huo na wakaomba ITV waungane na TBC kurusha mkutano wa JK live Jangwani. Safari ya ukombozi ni ndefu lakini lazima tuitembee.

Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimena mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika