Tuesday, October 26, 2010

DR SLAA AUNGURUMA MANZESE

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=15746&d=1288096234

Mkutano wa DR W P SLAA LIVE TOKA MwembeYanga

Nawakaribisha katika mkutano wa Mgombea uraisi kwa tiketi ya chadema DR W P SLAA unaofanyika hapa Kwenye uwanja wa Mwembe yanga watu wamejaa kweli kweli , kumefurika na kutia fora – Kuna watu wa aina mbalimbali hapa kuanzia wazee , vijana na wale watu wakati , kuanzia wamachinga mpaka wauza mitumba walioacha biashara zao kwa muda kwa ajili ya kuja kumwona dr slaa akinadi sera zake uwanjani hapa

Kwa wale walio mbali na maeneo haya wanafuatilia mkutano huu wanaweza kutazama TC1 Kuanzia saa 9 Kamili , wengine wanaweza kufuatilia kwa njia ya mtandao kama hii .

Kwa wale wanaopenda kuchangia Kampeni hizi wanaweza kutembelea blogu yetu kwa anuani www.marafikiwaslaa.blogspot.com kama una habari zaidi unaweza kututumia kupitia friendsofslaa@gmail.com

Wale wanaopenda kuchangia mkakati wa kutengeneza vipindi vya TV vinavyoendelea kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya TV na radio wanaweza kuchangia kupitia namba

+255766334049 MPESA
+255786806028 ZAP

Kama unataka Fulana za DR SLaa na Kofia zenye sahihi yake wasiliana na 0714 667026

dk slaa alivyounguruma zanzibar

Mgombea Urais kwa chama cha CHADEMA Dk Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wake wa kampeni wa lala salama, uliofanyika katika viwanja vya Garagaza,vilivypo Mtoni, Unguja, Zanzibar. (Picha na Emmanuel Herman).

Monday, October 25, 2010

Slaa kuunguruma Mwembeyanga

Napenda kuwafahamisha kuwa kesho Dr. Slaa atakuwa viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa LIVE ndani ya TBC1 pia kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa masaa 3.

Aidha, baadae atakuwa LIVE katika televisheni ya Agape kuanzia saa 1 jioni.

Mkutano wake leo umejaza watu wengi sana huko Zanzibar tofauti na wengi mnavyoweza kudhani, nitawaletea picha za Zanzibar hali ilivyokuwa.

DR SLAA AUNGURUMA ZANZIBAR


NUKUU ZA DR WP SLAA


  1. Monduli wanaishi maisha magumu.
  2. Tanzania bila CCM inawezekana, na kuendelea kukaa na CCM ni maafa makubwa.
  3. Kama ningesema uongo kuhusu ufisadi wa JK na waswaiba wake, mbona sichukuliwi hatua?
  4. Ukitukanwa, angalia, puuzia na uondoke. Ukipigwa kofi, mgeuzie na la pili...!
  5. Sipendi kwenda ikulu huku damu zikimwagwa, au kuwaacha watanzania wakiwa vilema kwa ajili yangu...!
  6. Nipo tayari kula mihogo ikulu, ili mtoto wa tanzania asome...!
  7. Siendi kuwa raisi wa Afrika Mashariki, bali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...!
  8. Kodi ya saruji kutoka Tanzania ni 18%, Kenya 15% na Uganda 16%....! Eti ndio makubaliano yaliyowekeana kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki...!
  9. Ninazo nyaraka kuwa serikali ya Tanzania imefanya partial payments huko Canada kwa ajili ya mabango ya CCM...!
  10. Sikatai kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini lazima tufanye maandalizi kuwapatia watanzania elimu itakayowawezesha kuingia kwenye ushindani...!

CHAGUA CHADEMA CHANGIA CHADEMA

Wakazi wa Kawe waliojitokeza kwa wingi leo jioni kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,Dk Slaa katika kampeni zake za lala salama.


Wakazi wa Kawe wakiwa katika viwanja vya Tanganyika Pekaz

Maelfu ya wakazi wa Kawe waliojitokeza