Wednesday, November 3, 2010

Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

http://mwananchi.co.tz/

0 comments:

Post a Comment